Aina hii ya tuzo hutambua watu binafsi au mashirika ambayo yanayokabiliana na hali iliyopo. Washindi katika nyanja hii huonyesha jinsi uendelevu wa mazingira unavyoendana na matumizi mazuri ya fedha.
Washindi wa tuzo la Mabingwa wa Dunia huchaguliwa na waamuzi wa kimataifa kufuatia mapendekezo yanayotolewa na umma. Kiwango kikubwa cha mapendekezo yanayotolewa ni ishara ya ongezeko la idadi ya watu wanaoelewa ni nini kinachowezekana na wanaona kuwa kuna fursa ya kutunza na kuboresha mazingira.
Masuluhisho yapo na watu na mashirika kutoka kote ulimwenguni wanajitolea kuyatekeleza. Mabingwa wa Dunia hukabiliana na majanga na wanathibitisha kwamba binadamu wana maarifa na nia ya kutunza na kuboresha mazingira yetu. Mabingwa huchaguliwa kwa mabadiliko yao chanya kwa mazingira na kwa uongozi wao wa kuhimiza hatua za ujasiri na madhubuti kwa manufaa ya sayari na wakaazi wake.