Showing 1 - 20 of 67
67 results found
Wakili na mwanachama wa Kabila la Asili ya Yurok la California, Amy Bowers Cordalis ametumia miongo kadhaa kujitahidi kurejesha mtiririko wa kiasili wa Mto Klamath nchini Marekani.
Watu na mashirika kote ulimwenguni wanaendeleza masuluhisho bunifu na endelevu ili kuboresha ardhi, kuimarisha ustahimilivu kwa ukame na kukomesha kuenea kwa majangwa. Mabingwa wa Dunia huwa mstari mbele, huku wakitoa matumaini na motisha kwamba uboreshaji wa ardhi unawezekana. Wanatukumbusha kwamba kulinda mazingira ni muhimu ili kufikia maendeleo endelevu.
Kisa cha SEKEM kinaanzia jangwani nchini Misri na hema, trekta na piano.Katika mwaka wa 1977, mwanzilishi wa shirika hili la maendeleo, Ibrahim Abouleish, alirudi nchini Misri baada ya miaka 20 ya kufanya kazi nje ya nchi katika kemia na famakolojia.
Watu kote ulimwenguni wanajitokeza na mbinu bunifu za kukomesha uchafuzi wa plastiki na kuboresha sayari yetu. Mabingwa wa Dunia wako mstari mbele kwenye juhudi hizi. Wanatupa matumaini kuwa kuna masuluhisho kwa uchafuzi wa plastiki na kutukumbusha kuwa uendelevu wa mazingira ni muhimu katika kufikia maendeleo endelevu.
Nairobi, Novemba22, 2022 – Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) leo lilitangaza washindi wake wa mwaka wa 2022 wa Tuzo la Mabingwa wa Dunia.
Cécile Bibiane Ndjebet (Cameroon), anayetuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ni mtetezi asiyechoka wa haki za wanawake za kumiliki ardhi barani Afrika, hali inayohitajika kuwawezesha kutekeleza wajibu muhimu wa koboresha mifumo ya ekolojia, kupambana na umaskini na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Dkt Purnima Devi Barman (India), anayetuzwa katika kitengo cha Maono ya Ujasiriamali, ni mwanabiolojia wa wanyamapori anayeongoza "Jeshi la Hargila", vuguvugu la wanawake pekee la uhifadhi mashinani linalojitolea kulinda Korongo aina ya Greater Adjutant Stork dhidi ya kuangamia.
Sir Partha Dasgupta (Uingereza), aliyetuzwa katika kitengo cha Sayansi na Ubunifu, ni mwanauchumi mashuhuri ambaye ukaguzi wake wa kipekee kuhusu uchumi wa bayoanuai unatoa wito kutafakari upya mno kuhusu uhusiano wa binadamu na mazingira asilia ili kuzuia mifumo muhimu ya ekolojia kuporomoka.
Constantino (Tino) Aucca Chutas (Peru), ambaye pia ametuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ameanzisha mfumo wa upandaji miti katika jamii unaoendeshwa na wenyeji na jamii za kiasili. Hali ambayo imepelekea miti milioni tatu kupandwa nchini Peru. Pia anaongoza juhudi kabambe za upandaji miti katika nchi zingine za eneo la Andes.
Arcenciel (Lebanon), kampuni inayotuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ni shirika linalokuza mazingira safi na bora na kuchangia msingi wa kuwekwa kwa mkakati wa kitaifa wa kushughulikia taka nchini Lebanon. Kwa sasa, arcenciel huchakata zaidi ya asilimia 80 ya taka za hospitali zinazoweza kuambukiza magonjwa nchini Lebanon kila mwaka.
Mabingwa wa Dunia hushughulikia mazingira kwa njia bunifu ili kuyawezesha kujiboresha kwa njia za kipekee. Awamu ya mwaka wa 2022 inaangazia juhudi za kuzuia, kusitisha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia kote ulimwenguni.
Thank you for subscribing.
Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa hujivunia kufanya kazi na wabia kutambua na kusherehekea mafanikio ya kipekee ya washindi wa tuzo la Mabingwa wa Dunia. Ni kutokana na ukarimu wao mkuu ndipo tunapoweza kuendelea kusherehekea mafanikio yao. Wabia wetu hufadhili juhudi za Mabingwa wa Dunia na Vijana Bingwa Duniani. Weibo
Washindi saba wa tuzo za Dunia walitangazwakatika mwaka wa 2018.
Showing 1 - 20 of 67