Search Results

Showing 41 - 60 of 64

64 results found

Nairobi, January 20, 2020 – Kupendekeza washiriki wa mwaka wa 2020 wa  tuzo la Mabingwa wa Dunia, tuzo la ngazi ya juu linatolewa na Umoja wa Mataif

Categorized Under: Global

Patagonia imepokea tuzo  linalotolewa na Umoja wa Mataifa kwa heshima ya mazingira kutokana na kuwa na  maono ya ujasiriamali. Patagonia imetuzwa kutokana na kujitolea kwake kuhakikisha uendelevu na kufanya uhamasishaji ili

Leyla Acaroglu alikuwa na umri wa miaka 19 wakati wake wa kwanza kuhudhuria somo la kubuni michoro. Alisikia kitu ambacho kilibadili mtazamo wake kuhusu dunia milele.

Raia wa Kanada, mwanasayansi wa masuala ya hali ya hewa, Profesa Katharine Hayhoe ndiye mshindi wa Tuzo la Bingwa wa Dunia lilnalotolewa na Umoja wa Mataifa, katika kitengo cha sayansi na ubunifu. Ametuzwa kutokana na ujuzi wake na kw

Costa Rica yashinda tuzo muhimu la mazingira linalotolewa na Umoja wa Mataifa katika kitengo cha sera na uongozi Nchi kotoka Amerika ya Kati imetuzwa kwa kuwa mstari mbele kuhakikisha kutokuwepo kwa hewa ya ukaa siku zijazo

Motisha Na Kuchukua Hatua

Mkoa wa Zhejiang ulipata jina lake kutoka kwa Mto Zhe, kwa maana ya mto "usionyooka" au "uliopinda". Mito katika mkoa wa Zhejiang ina umuhimu kwa jamii kutoka kitambo, inatiririka kupitia miji ya zamani, kati ya nyumba za jadi zilizo na kuta nyeupe na paa nyeusi, na hunufaisha mashamba ya mpunga.

Uongozi wa sera

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa linamutambua Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwa uungozi wake wa kishujaa kuhusiana na masuala ya mazingira katika ngazi ya kimataifa. Chini ya uongozi wa Narendra Modi, India iliahadi kukomesha matumizi ya plastiki zinazotumiwa tu mara moja katika nchi hiyo kufikia mwaka wa 2022.

Mafanikio Ya Kudumu

Joan Carling amekuwa akipigania haki za ardhi na za mazingira ya watu wa kiasili kwa zaidi ya miaka 20. Alishiriki kikamilifu katika Jukwaa la Mapatano la Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na REDD+. Amefanya kazi kama Katibu Mkuu wa Mkataba wa Watu wa Asili ya Asia mara mbili. Pia alikuwa mwenyekiti wa Muungano wa Watu wa Cordillera.

Sayansi Na Ubunifu

Impossible Foods na Beyond Meat walishinda kwa pamoja Tuzo la Mabingwa wa Dunia, katika kitengo cha Sayansi na Ubunifu. Wanatoa vibadala vya kudumu kwa baga za nyama ya ng'ombe ambavyo ni rafiki zaidi kwa mazingira na vinatoa ushindani kwa ladha ya nyama.

Uongozi wa sera

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amelipa swala la utunzaji wa mazingira kipau mbele katika ajenda yake ya nchi za kigeni. Anatambuliwa kwa kupigania kuwepo kwa Muungano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua na kukuza ushirikiano wa kimataifa ili kushughulikia masuala ya mazingira, na kwa uongozi wake kuhusiana na Mkataba wa Kimataifa wa Mazingira.

Maono Ya Ujasiriamali

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cochin ni uwanja wa ndege wa kwanza kutumia nishati ya jua duniani. Hutekeleza kazi zake zote kwa kutumia nishati ya jua. Ni uwanja wa ndege mkubwa zaidi na wenye shughuli nyingi zaidi katika jimbo la Kerala nchini India, na pia ni uwanja wa ndege wenye shughuli nyingi zaidi nchini India kwa kuzingatia mlolongo wa ndege za kimataifa.

Paul A. Newman na Kituo cha NASA’s Goddard Space Flight Center ni Bingwa wa Dunia wa mwaka wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa katika kitengo cha Sayansi na Ubunifu na kutokana na mchango wao wa kipekee kwa Mkataba wa Montreal- ambao umepunguza vitu vinavyoharibu ozoni kwa asili mia 99 na kusababisha tambiko la ozoni kuboreka.

Jamii ya upandaji miti ya Saihanba, ni Bingwa wa Dunia wa mwaka wa 2017 wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa kutokana na kufanya ardhi iliyoharibika kuzalisha miti mingi.

Wang Wenbiao, Mwenyekiti wa Kikundi cha Elion Resources Group ni Bingwa wa Dunia wa mwaka wa 2017 kutokana na mafanikio yake ya kudumu.

Mobike ni Bingwa wa Dunia wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa kutokana na maono yake ya ujasiriamali ya kutoa suluhisho kwa uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuzingatia soko.

Mshindi wa tuzo la utengenezaji filamu, Jeff Orlowski, ni Bingwa wa Dunia wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa kutokana na mafanikio yake ya kutuma jumbe nzito kuhusiana na mazingira kwa watazamaji kote ulimwenguni.

Michelle Bachelet, Rais wa Chile, ni Bingwa wa Dunia wa mwaka wa 2017 kutokana na uongozi wake wa kipekee wa kuunda maeneo ya bahari yaliyohifadhiwa na kukuza nishati jadidifu.

Katika video hii fupi, tazama wakati muhimu kabisa wa Maonyesho ya Tuzo la Mabingwa wa Dunia la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa yalioendeshwa na Dia Mirza na Alec Baldwin na yaliyofanyika Septemba 26, 2018 katika mji wa New York City.

Tuzo la Mabingwa wa Dunia hutuza watu binafsi na mashirika ambayo huchukua hatua za kusababisha mabadiliko chanya kwa mazingira. UNEP inatafuta kupendekezwa kwa watu binafsi na mashirika yanayofanya kazi kupata masuluhisho bunifu na endelevu ya kuboresha ardhi, kuimarisha ustahimilivu kwa ukame, na kupambana na kuenea kwa majangwa. 

Showing 41 - 60 of 64