Likiendelezwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA) huleta pamoja wawakilishi kutoka kwa Nchi Wanachama wa UN 193, mashirika ya biashara, viongozi wa mashirika ya uraia, na wadau wengineo ili kukubaliana kuhusiana na baadhi ya sera zitakazokabiliana na changamoto za mazingira ulimwenguni.
Kikao cha tano cha UNEA kitaendeshwa ifuatavyo:
-
Kikao cha mtandaoni cha UNEA-5 ni tarehe 22 na tarehe 23 mwezi wa Februari 2021.
-
Mkutano wa ana kwa ana wa UNEA-5 utafanyika mjini Nairobi katika mwezi wa Februari mwaka wa 2022.
Kauli mbiu ya vikao vyote viwili vya UNEA-5 ni “Kuimarisha Juhudi za Kushughulikia Mazingira ili Kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”. Inaonyesha umuhimu wa mazingira kwa maisha yetu na kusababisha maendeleo endelevu kwa kwa jamii, uchumi na mazingira. Mazingira ni muhimu ili kufikia Ajenda 2030 iliyokubaliwa na nchi zote wanachama wa UN katika mwaka wa 2015. Ajenda 2030 inalenga kusitisha umaskini na mizozo, kujenga jamii yenye haki na usawa, na kuhakikisha kuwa sayari na malighafi zinatunzwa daima. Malengo 17 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ni mfumo wa jinsi nchi zinaweza kufikia ajenda hii.
Ikijawa na uanwai na kuwa changamano, mazingira ni msingi wa chumi zetu na jamii zetu. Binadamu wanaharibu huduma hizi zinazowezesha maisha kupitia kwa kuzitumia kupindukia, kutotahadhari wakati wa kufanya maendeo na mabadiliko ya tabianchi. Kwa pamoja, tunahitaji kutunza na kuboresha dunia yetu asilia.
Vielelezo vinaonyesha kuwa kutekeleza sera zitakazowezesha matumizi endelevu ya rasilimali, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kupunguza uharibifu wa bayoanuai kunaweza kuongeza Pato La Jumla la Taifa (GDP) kwa asilimia 8 huku uzalishaji wa gesi ya ukaa ukipunguzwa kwa asilimia 90 kufikia mwaka wa 2060. Kurudishwa kwa hali halisi ya hekta milioni 350 ya ardhi iliyoharibiwa na mifumo ya ekolojia ya majini itaboreshwa kati ya sasa na mwaka wa 2030, tunaweza kupata dola za marekani trilioni 9 kutokana na huduma kutoka kwa mifumo ya ekolojia.
Mikakati ya kujiimarisha baada ya janga la COVID-19 inayowekeza kwa mazingira na ajira zisizochafua mazingira, mifumo endelevu ya fedha, ushughulikiaji mwafaka wa kemikali, uzalishaji na utumiaji wa bidhaa kwa njia endelevu
UNEA-5 inatoa fursa kwa Nchi Wanachama kushiriki njia bora za kuwezesha maendeleo endelevu. Itawezesha serikali kujiimarisha vyema baada ya korona kwa kutunza mifumo ya ekolojia na kupitia masuluhisho yanayotokana na mazingira.