Mifumo ya chakula ni muhimu kwa binadamu, wanyama, uchumi na kwa mazingira. Ardhini na baharini mifumo yetu ya chakula na maji safi hutegemea malighafi, ila ongezeko la idadi ya watu, mabadiliko ya lishe kutokana na kuongezeka kwa utajiri na uchafuzi unaotokana na kilimo ni vitu vinavyoharibu malighafi kwa haraka kuliko uwezo wake wa kuzalisha. Mifumo yetu ya chakula huchangiarobo ya jumla ya uzalishaji wa gesi ya ukaa unaofanywa na binadamu.
Idadi ya watu duniani inatarajiwa kufikia bilioni kumi kufikia mwaka wa 2050. Kuhakisha kuwa kuna chakula cha kutosha, chenye lishe bora ni sharti tufanye mabadiliko makuu kwa jinsi tunavyopanda, zalisha na kusafirisha chakula chetu.
Dunia hutumia takribani dola milioni 1 kwa dakika kama ruzuku ya kilimo. Kubadilisha matumizi ya ruzuku, uwekezaji na motisha ya kuvifanya endelevu na kuzalisha chakula kwa njia endelevu kutoka kwenye mashamba na bahari kunaweza kutosheleza mahitahi ya chakula kwa vizazi vijavyo.
Kilimo endelevu ni ukulima uaozalisha faida, kutunza mazingira na kuwa na manufaa kwa jamii na uchumi. Hujali mifumo ya ekolojia na kuwezesha kiwango kikubwa cha bayoanuai kwa kuboresha makazi muhimu ya kiasili. Kilimo endelevu pia huboresha hali ya hewa. Hutumia nguvu kidogo kwa asilimia 56 za kuzalisha kila mmea, na kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa kwa zaidi ya asilimia 60 kwa hekta ikilinganishwa na kilimo kilichopo.
Uzalishaji wa chakula kwa njia endelevu huimarisha utoshelezaji wa chakula na kusaidia kufikia malengo ya kimataifa, kama vile Malengo ya Maendeleo Endelevu Kutokomeza Njaa.