Ukuaji wa uchumi dhabiti hutegemea mifumo ya ekolojia. Kuanzia kwa misitu hadi kwa mashamba ya kilimo, mifumo ya ekolojia duniani ni chanzo cha rasilimali, huduma na viwanda. Ila idadi ya watu duniani inapoendelea kuongezeka maradufu, na kuongeza mahitaji, mandhari haya yanaharibiwa kwa kiwango cha kutisha.
Ikishughulikiwa ipaswavyo, mazingira yanaweza kuwa nguzo muhimu ya kukomesha umasikini, kutoa kipato na kukuza uchumi kwa mda mrefu.
Hii inamaanisha kuleta maendeleo bila kuharibu mazingira. Inamaanisha kutumia malighafi kikamilifu na kutumia tena na tena ili kuendelea kutumia vitu vilevile tena wakati wa mchakato wa uzalishaji.
Kuwekeza kwenye utunzaji na uboreshaji wa mifumo ya ekolojia kutasaidia kukinga binadamu dhidi ya gharama na madhara makubwa yanayoweza kutokea kutokana na majanga ya baadaye na mabadiliko ya tabianchi.
Kujiimarisha baada ya COVID-19 ni fursa inayotokea mara moja duniani ili kukabiliana na madhara tunafanyia mazingira. Fedha za kujiimarisha baada ya korona zinazotengwa na serikali kadhaa zinapaswa kuwezesha mazingira endelevu. Zinapaswa kuwezesha matumizi ya malighafi kikamilifu, ushughulikiaji mzuri wa taka, upunguzaji mkubwa wa uchafuzi na uzalishaji wa gesi chafu.
Kujiimarisha kwa kupunguza kiwango cha gesi chafu inayozalishwa, huku afya ya binadamu ikiimarishwa, na kuboresha miji na majiji yetu, na kutunza mazingira kwa vizazi vijavyo.