Dunia inaendelea kushuhudia ongezeko la joto zaidi kuliko kipindi kingine chochote kwenye historia. Wastani wa kiwango cha joto duniani kwa sasa ni nyuzijoto 1.1°C zaidi ikilinganishwa na mwanzoni mwa karne iliyopita. Iwapo kiwango cha joto kitaendelea hivyo bila kudhibitiwa, itakuwa na madhara mabaya mno kwa binadamu, kwa ekolojia na kwa uchumi, na kusababisha uhaba wa chakula, mioto mikuu, kuongeza urari wa bahari na kusababisha hali mbaya mno ya hewa.
Uzalishaji wa gesi ya ukaa usipopunguzwa kwa asilimia 7.6 kila mwaka kati ya 2020 na 2030, dunia haitaweza kufikia nyuzijoto 1.5 za kiwango cha joto zinazolengwa kufikiwa chini ya Mkataba wa Paris.
Kuboresha na kutunza mazingira ardhini na baharini ni mojawapo ya mikakati mikuu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Misitu, maeneo oevu, na mifumo mingine ya ekolojia ni muhimu katika kukabiliana na hali mbaya ya hewa, kutunza makaazi, mimea, usambasaji wa maji na miundo msingi. Kuhifadhi na kuboresha mifumo hii muhimu ya ekolojia kutasaidia kudumisha sayari dhabiti tunapojenga jamii zetu na chumi zetu baada ya janga hili la COVID-19 .
Ripoti ya UNEP ya 2020 Emissions Gap ilionyesha kuwa kujiimarisha baada ya janga la korona kunaweza kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa kwa asilimia 25 ilivyotabiriwa kufikia mwaka wa 2030 na kuwezesha dunia kuwa karibu kufikia nyuzijoto 2 zinazolengwa chini ya Mkataba wa Paris kuhusiana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Viwango, sera na sheria za kuzuia uzalishaji zaidi wa gezi chafu ni muhimu. Kwa mfano, katika mwaka wa 2020, Nchi 15 za Afrika zilitangaza sheria mpya kuhusu uchafuzi wa magari na matumizi ya fueli kikamilifu. Nchi pia zinahitaji kukomesha ruzuku zinazotolewa kwa fueli za visukuku na kuwekeza kwenye teknolojia zilizo na uwezo mdogo wa kuzalisha gesi chafuzi, kuwekeza kwenye nishati jadidifu na miundo msingi isiyochafua mazingira.
Kila iwezekanavyo, bajeti ya kila mwaka itengwe ili kuzuia mdororo wa uchumi ulimwenguni na iende sambamba na Malengo ya Maendeleo Endelevu na Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi.