Ebola, SARS, Zika, VVU/UKIMWI, homa ya West Nile na sasa COVID-19. Haya ndiyo baadhi ya magonjwa makuu yalishuhudiwa katika miongo kadhaa iliyopita. Ijapokuwa yalianzia sehemu mbalimbali duniani, yana sifa moja. Ndiyo yanayorejelewa na wanasayansi kama “zoonotic diseases,” magonjwa yanayoambukizwa binadamu kutoka kwa wanyama, baadhi yakisababisha magonjwa na vifo yanapotokea.
Magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama yameathiri jamii tangu zama za kale. Idadi ya watu ulimwenguni inapoelekea kufikia bilioni 8, maendeleo yasiyodhibitiwa, uharibifu na matumizi ya mazingira visivyo ni hali inayoongezo uwezo wa wanyama na binadamu kusongeana, hali inayofanya magonjwa haya kuenea kwa urahisi.
Uchafuzi pia ni hatari. Kila mwaka, watu bilioni tisa huaga mapema kutokana na uchafuzi kwa hivyo jinsi tunavyoshughulikia taka ni muhimu kwa sababu kwa sababu ina athari ghasi kwa afya na kwa uchumi.
Uwezo wetu wa kupunguza uwezekano wa majanga mengine kutokea katika siku zijazo na kukinga afya ya watu dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuiliwa yanayotokana na uchafuzi unaweza kuimarishwa kwa kusitisha uharibifu wa maeneo ya makaazi na kwa kutunza na kuboresha mifumo ya ekolojia. Na kuyazuia si ghali kuliko ufadhili wa kukabiliana na hali baada ya janga la kiafya.
Mbinu ya One Health inaangazia kila kitu kuhusiana na afya ya binadamu, ya wanyama na hali bora ya mazingira ili kudhibiti chanzo na usambaaji wa magonjwa tandavu. Sera na ubajeti ya uwekezaji ya kila mwaka zinaweza kuimarisha uhusiano kati ya afya ya binadamu na hali ya mifumo ya ekolojia, kwa kutoa kipaumbele kwa kutunza na kuboresha mazingira kwa sababu tunapotunza mazingira, mazingita hututunza.