03 Oct 2019 Tukio Kutumia mazingira kushughulikia tabianchi

Kushauriana ni njia mwafaka ya kukabiliana na changamoto kuu ili kuboresha ardhi iloyoharibika

Dunia inakabiliana na changamoto kuu mno za bayoanuai na za mabadiliko ya tabianchi. Njia moja ya kukabiliana na hali hii ni kuboresha ardhi iliyoharibika.

Uboreshaji wa mandhari- ukifanya vizuri kwa ushirikiano na jamii za kiasili, serikali na wanasayansi- una manufaa mengi kwa mazingira, ukabilianaji wa tabianchi na ya kiuchumi. Pia huchangia zaidi katika nyingi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Mradi wa tangu mwaka wa 2015 hadi 2019 wa Mfuko wa Mazingira Duniani  Unaoweka msingi wa kuboresha mandhari ya misitu kwa kiwango kikubwa, ulioanzishwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)na kutekelezwa na Taasisi ya Rasilimali Duniani  (WRI) kwa ushirikiano na mataifa matano (Ethiopia, India, Indonesia, Kenya na Niger) ni muhimu katika uboreshaji wa mandhari.

"Hakuna njia moja tu  ya  kuboresha ardhi iliyoharibika, bila kuzingatia vipengele mbalimbali-vya kitamaduni, vya kijamii, vya kiuchumi na vya kitopografia-vinavyojitokeza katika nchi na maeneo mbalimbali," asema  Ulrich Piest, mtaalamu wa UNEP wa mifumo ya ekolojia. "Ijapokuwa kupanda miti ni muhimu ili kuboresha mandhari, siyo kazi rahisi."

Mradi huu unawezesha uwajibikaji katika ngazi ya kitaifa kwa kuwezesha utungaji wa sheria bora na kuweka mikati bora katika sekta mbalilimbali. Lengo kuu: kukuza upanzi wa miti katika maeneo ya kilimo, na kupanda misitu tena kwa njia zinazokuza mikakati ya kuepuka ukataji wa miti na kukuza kilimo cha kisasa kinachojali mazingira.

"Uwekezaji katika kuboresha ardhi una manufaa mengi ya kiuchumi na kwa jamii hasa misitu inapotunzwa. Lakini mikakati ni sharti ijumuishe watu wote muhimu wanaohusika ili kufaulu," anasema  Fred Stolle, mratibu wa mradi. "Mchango wa viongozi wa jamii, makampuni, ngazi mbalimbali za serikali, wanasayansi na mafundi hutoa taarifa muhimu zinazowezesha kufanya maumuzi  muhimu na kutajirisha watu wanaoishi vijijini.

India

Nchini India, asilimia 70 ya umma hutegemea kilimo na asilimia 82 ni wakulima wadogowadogo,ila sehemu kubwa ya ardhi yao imeharibika. Mtandao wa kipekee wa kwanza, Restoration Opportunities Atlas, unakadiria kuwa takribani hekta milioni 140 ya mashamba zinaweza kuboreshwa na kutunzwa nchini India. Uzoevu wa kutosha wa maendeleo katika maeneo ya mashambani nchini humo,  maeneo ya maji na utunzaji wake vimewekwa kwenye Atlasi kutokana na mradi huo. Pia mradi uliwezesha kuwekwa kwa mikakati ya kuboresha mandhari katika Wilaya ya Sidhi, katika jimbo la Madhya Pradesh. Takribani shamba hekta 360,000 wilayani liliweza kuboreshwa kwa kutekeleza mikakati ya uboreshaji ipatayo 8.

"Iwapo uboreshaji utatekelezwa kwa kuzingatia yale tuliyojifunza kupitia mradi huu na kupitia kwa ushauri, nafasi 30,000 za kazi zinaweza kubuniwa kupitia kwa aina sita ya miradi itokanayo na miti. Inaweza sababisha watu milioni 3.75 kupata ajira na kipato cha dola za Marekani milioni 10 kama mshahara kwa jamii asilia," asema Ruchika Singh, kutoka WRI nchini India.

Kenya

Nchini Kenya mradi ulitekelezwa katika eneo kame kwa Kaunti ya Makueni, iliyo na idadi ya watu wapatso milioni moja. "Ilikuwa muhimu kushauriana na wenyeji hasa katika wadi ili kubaini mbinu mwafaka ya uboreshaji itakayokubalika na yenye manufaa kwa idadi kubwa ya watu," asema Mary Mbenge, Afisa Mkuu wa Mali Ghafi, Mazingira na Mabadiliko ya tabianchi. "Tulisahuriana nao kupitia kushirikisha umma kwa mijadala, kupitia ushirikiano na serikali ya kaunti, ili kupata njia mwafaka ya uboreshaji."

"Degraded land (foreground) and landscape being restored (background) in Makueni County, Kenya  Photo by Peter Irungu/World Resources Institute"

Ethiopia

Setilaiti za Google Earth zilitumiwa katika Wilaya mbili nchini  Ethiopia, siyo tu kuelewa jinsi upandaji wa miti hubadilika na wakati bali pia kutoa taarifa ya utekelezaji wake nyanjani.  Lengo lilikuwa ni kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa, kuwa na chakula cha kutosha, na kuzuia uharibifu wa mito kupitia kwa upanzi wa miti, upandaji wa miti maeneo yaliyokatwa, upandaji wa miti katika maeneo ya kilimo, upandaji wa miti kando ya barabara na kandokando ya mito na kuchukua hatua za kukomesha mmomonyoko wa udongo. Ijapokuwa haya yametekelezwa kwa miaka mingi nchini  Ethiopia, wafanya maamuzi wilayani sasa wanaweza kushiriki data ya utekelizaji kutoka kwa  picha za setilaiti ili kuimarisha juhudi za uboreshaji.

"Restoration intervention in Tigray, Ethiopia  Photo by Aron Simen/World Resources Institute"

Niger

Katika nchi ya Niger, watu wanamiliki mashamba na wala si miti ipatikanayo katika mashamba hayo, kwa hivyo hawaoni manufaa ya kupanda miti isiyokuwa yao. Katika hali iwayo yoyote, ushauri  kutoka kwa wadau unahitajika ili kupata maoni ya wenyeji, ya kitaifa na ya kikanda kufanikisha mradi wa upandaji wa miti. "Changamoto zilizopo za kisheria  nchini Niger zinaweza kutatuliwa hivi karibuni kutokana uongozi katika ngazi ya kitaifa kutokana na mbinu ya kupanda miti tena kutokana na mradi," anasema WrI’s Salima Mahamoudou, anayefanya kazi nchini Niger.

"Consulting with the community to build restoration plan, Lido Village in Niger  Photo by Salima Mahamoudou"

Ni vigumu koboresha mandhari ya Niger lakini taifa hilo limefaulu kupata mafanikio kwa kujenga sehemu ya ukuta wake wa Great Green Wall  na kunachangia katika mafanikio ya mradi wa African Forest Landscape Restauration Initiative(AFR100). Hii inadhihirisha kuwa upandaji wa miti na miradi mingine ya kuiboresha inawezekana iwapo sekta za kibinafsi, serikali na wenyeji watahusishwa.

Kwa miongo sasa, wakulima wengi kutoka Niger walikata matawi na mizizi iliyoota kwa miti iliyokatwa ili kurutubisha mchanga na mimea. Lakini miaka 15 iliyopita, Sakina Mati na Ali Neno Malam waliamua kujaribu kufanya jambo geni. Walianza kukuza mimea hiyo, kwa kuhifadhi ile iliyo na afya  na kukata mingineyo. Ukataji wa aina hii na utunzaji wa miti michanga, unajulikana kama  kusaidia miti kujikuza, na huwezesha matawi mapya kumea na mingine kuotesha mizizi iliyojificha. Inawezesha mizizi kuvuta maji chini ya ardhi na kusaidia mimea kupata maji na kusaidia mchanga ulio na rutuba.

"Miaka 15 iliyopita, sikuwa na miti shambani mwangu, na nililazimika kwenda kutafuta mafuta taa ya kupikia kila siku kwa sababu tulikosa kuni," Sakina Mati alielezea kikosi kinachosimamia mradi. "Lakini leo, kuna zaidi ya miti 150 shambani mwangu." Hatua za kuongeza kijani zilizoongozwa na Sakina Mati, Ali Neno na wanakijiji wengine, zimewawezesha kuwa na kuni, chakula cha wanyama-na mbao nyingi zinazopatikana zilipelekea kufunguliwa kwa kwa soko la mbao kwa jamii jirani.

Indonesia

"Upanzi wa miti katika maeneo ambayo yamekatwa miti ambayo haijaoza siyo njia mwafaka ya kuboresha mashamba nchini  Indonesia," asema Hidayah Hamzah, mchanganuzi wa masuala wa  WRI aliyeshiriki katika mradi. Uboreshaji wa mandhari nchini Indonesia, kama kwengineko, hukumbwa na changamoto za kijamii na za kiuchumi: mashamba yaliyo na miti iliyokatwa na haijaoza yanahitaji kumwagiliwa maji  au kuwa karibu na mikondo ya maji kwa sababu yakishika moto, huzalisha kiwango kikubwa cha kabonidiokisidi. Mashauriana yalichukua nafasi muhimu wakati wa kukusanya hizi taarifa.

Funzo

"Mradi huu umetoa mafunzo muhimu kwetu," anasema Mahamoudou.

"Tumejifunza kuwa shughuli ya upandaji wa miti ni sharti zinufaishe nchi nzima na ni sharti  wenyeji washirikishwe. Serikali na wafadhili wanapaswa kuelimishwa kuhusu manufaa  kwa uchumi na kwa jamii. Kabla ya kuanza shughuli ya uboreshaji wa mandhari, ni vyema  kubainisha wahusika wakuu ili kufanikisha mradi. Miradi ya kipindi kifupi siyo mwafaka," anaongezea.

Kuboresha ardhi iliyoharibika ni sehemu tu ya yale yanayohitajika. Tunapaswa kuepuka uaribifu wa mashamba, kwa kushughulikia suala hili na kwa kuchukua hatua mwafaka za kuzuia mabadiliko yatakayoathiri hali ya ardhi ambayo bado haijaharibika na kuiwezesha kustahimili, kupitia sheria mwafaka na sera za utunzaji.

Uharibifu kwa ardhi unaweza pia kupunguzwa au kukabiliana nao kupitia mashamba ya kilimo na yale ya misitu kupitia shughuli zinazosababisha uendelevu.

"Pale inapowezekana, baadhi (na kwa nadra yote) ya uwezo wa uzalishaji na huduma za ekolojia zinaweza kuboreshwa kupitia kwa kusaidia mifumo ya ekolojia kufanya kazi vizuri," anasema Piest. "Na hapa ndipo mradi huu unakuwa wa muhimu."

 Karne ya Umoja wa Mataifa ya Kuboresha Ekolojia ya mwaka wa  2021 hadi 2030,ukiongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na washirika kama vile Afri100, the Global Landscapes Forum na the International Union for the Conservation of Nature, hushughulikia ekolojia za maeneo ya bara  na za maeneo ya pwani . Mwito wa kushughulikia suala hili duniani, utaleta pamoja wanasiasa, watafiti wa kisayansi na wafadhili  ili kuharakisha urekebishaji na uhifadhi. Tusaidie kuboresha karne.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Fred Stolle: fred.stolle@wri.org