UNEP/Duncan Moore
19 Jul 2021 Tukio Fresh water

Mabadiliko ya tabianchi yasababisha mafuriko kwenye ziwa kubwa mno jangwani: utafiti mpya

UNEP/Duncan Moore

Kwa miaka mingi ilionekana kama Ziwa Turkana, linaloptikana katika eneo kame Kaskazini mwa Kenya, lilikuwa linakauka.

Mito mikuu inayolisambazia maji ilikuwa imeathiriwa na mabwawa na watu wengi waliogopa kuwa kiwango cha maji kingepungua kwa thuluthi tatu, na kufanya Ziwa hilo kujigawa kwa mito miwili midogo. Lilikuwa, kwa mjibu wa ripoti moja, “Janga la Bahari za Visiwa janga la Kiafrika” – ambapo ni asilimia 10 tu eneo halisi la bahari limesalia.

Lakini utafiti mpya kutoka kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) linakisia kuwa maji yataongezeka kwenye Ziwa Turkana – na itakuwa hatari mno kwa watu milioni 15 wanaoishi katika mwambao wake.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kwa kipindi cha miaka 20 ijayo, mabadiliko ya tabianchi yanaweza kusababisha mvua kubwa, hali itakayosababisha kiwango cha maji kuongezeka na kuongeza uwezekano wa mafuriko mabaya zaidi kutokea.

Utafiti huo ilitoa wito kwa maafisa wa ngazi za juu nchini Kenya na Ethiopia, ambayo mipaka ya Ziwa Turkana hufikia, kujitayarisha kwa hatima ambayo mafuriko kama yale yaliyoshuhudiwa katika miaka ya na 2019 na 2020, yanayotokea kwa nadra, yatatokea mara kwa mara.

"Watu wengi hudhani kuwa mabadiliko ya tabianchi ni tatizo litakalojiri baadaye," anasema Frank Turyatunga, Naibu wa Mkuu wa UNEP,  Ofisi ya Afrika. "Lakini jinsi ambavyo ZiwaTurkana linavyoonesha, linatokea sasa na hata kulazimisha watu kujifunza kuishi na hali hiyo."

Ziwa Turkana, ziwa kubwa zaidi duniani jangwani, ni sehemu ya bonde la Omo-Turkana, linaloenea hadi katika nchi nne: Ethiopia, Kenya, Sudan Kusini na Uganda. Bonde hilo ni makazi ya mimea na wanyama wengi wanaopatikana kwa nadra.

Tangu mwaka wa 1988, nchi ya Ethiopia imejenga mabwawa mengi ya umeme unaotokana na maji kwenye tawimto lake, Mto Omo, hali inayosababisha ubashiri wa kifo cha Ziwa Turkana.

Bado kuna dhana nchini Kenya kwamba viwango vya maji ya ziwa hupungua kila wakati, hali inayofanya upangaji kuwa mgumu.

Tito Ochieng, Mkurugenzi wa Maji, Kaunti ya Turkana (Kenya)

 

Makadirio ya hali ya hewa

Kutumia mfano wa wa uchanganuzi wa hali ya juu wa rasilimali za maji na mabadiliko ya tabianchi, ripoti mpya ya UNEP iligundua kuwa hadi makazi nane ya watu karibu na ziwa hilo yanaweza kukumbwa na mafuriko mara kwa mara. Wakati mafuriko makubwa, ya ghafla yamekuwa nadra, makadirio ya mabadiliko ya tabianchi inakisia hali hii itatokea mara kwa mara na kuathiri watu wengi ikiwa mikakati ya kukabiliana nayo hazitawekwa.

Ripoti hiyo ilitoa wito wa kuboreshwa kwa ushirikiano wa kimataifa na mikakati ya kukabiliana na na hali, ikiwa ni pamoja na upandaji miti, kilimo cha misitu na kuzuia ujenzi katika maeneo yaliyo katika hatari ya kukumbwa na mafuriko.

"Katika miaka miwili iliyopita, kuongezeka kwa kiwango cha maji katika Ziwa Turkana kumeharibu maeneo ya kulisha mifugo, kufurika kwa majengo na kulazimisha watu kukimbia makazi yao," anasema Tito Ochieng, Mkurugenzi wa Maji katika Kaunti ya Turkana nchini Kenya. "Lakini Bado kuna dhana nchini Kenya kwamba viwango vya maji ya ziwa hupungua kila wakati, hali inayofanya upangaji kuwa mgumu."

Utafiti huo pia unaonyesha ushahidi wa kuongezeka kwa kiwango cha maji katika maziwa nane yanayopatikana kwenye Bonde la Ufa nchini Kenya. Mafuriko makubwa katika maziwa hayo katika miaka ya 2019 na 2020 yaliharibu nyumba na miundomsingi - na hata inasemekana yalisababisha kuongezeka kwa mashambulizi mabaya ya mamba.

Afrika inadhihirika visivyo kama eneo lililo hatarini mno kukumbwa na mabadiliko ya tabianchi. Hatari hii inasababishwa na viwango vya chini vya ukuaji wa uchumi katika jamii barani. Ijapokuwa mabadiliko ya tabianchi ni hali ya kimataifa, maskini wamo hatarini mno kuathirika.

Kazi ya UNEP ya kushughulikia mabadiliko ya tabianchi barani Afrika inasaidia nchi kutekeleza ahadi zao za kushughulikia mazingira - Ahadi Zinazotolewa na Nchi (NDCs) - kukidhi utoshelezaji wa chakula, kubuni mapato na nafasi za kazi kwa vijana, na ukuzaji wa uchumi.

Ushirikiano wa Kikanda

Ripoti hiyo ilikuwa sehemu ya mradi mpanaulioanzishw akuimarisha ushirikiano katika maeneo ya mipaka kati ya Ethiopia, Kenya na Somalia.

Mradi huo pia ulikuza chanzo wazi cha  eneo la taarifa kwenye bonde hilo, kwa kiasi fulani kikitegemea picha za setilaiti. Kina data kuhusu mimea kwenye ardhi, ubora wa maji na unyevu wa mchanga, na huchunguza hali anuwai za mabadiliko ya tabianchi.

Ripoti hiyo inatolewa baada ya kuzinduliwa kwa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia 2021-2030, juhudi za kimataifa za kukufua mazingira asili. Pia ni sehemu ya kazi pana ya UNEP ya kufuatilia na kuboresha mifumo ya maji safi kote ulimwenguni, kuunga mkonoLengo la Maendeleo Endelevu la 6.

 

Ripoti hii mpya kuhusu Ziwa Turkana ni sehemu ya "Msaada wa Kuwezesha Ushirikiano Mwema na Uratibu wa Miradi ya Inayovuka Mipaka ya Kusini Magharibi mwa Ethiopia na Kaskazini Magharibi mwa Kenya, Marsabit-Borana na Dawa, na mradi wa Kenya-Somalia-Ethiopia (SECCCI)". Ilifadhiliwa kwa kwa ushirikiano wa Mfuko wa Muungano wa Ulaya wa Dhamana ya Dharura kwa Afrika, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na UNEP na kutekelezwa na UNDP, UNEP, na  Mamlaka ya Kimataifa ya Maendeleo. Kama sehemu ya mradi wa miaka mitatu, uliokamilika Februari ya 2021, UNEP ilisaidia Ethiopia na Kenya kufanya kazi pamoja ili kusimamia vyema rasilimali zao za maji, na kusaidia mifumo ya ikolojia inayovuka mipaka kupitia ufuatiliaji wa mazingira na kukuza ushirikiano wa pande zote husika.

Kwa taarifa zaidi, wasiliana na Joakim Harlin: joakim.harlin@un.org