Mahojiano na Richard Munang, mtaalamu wa masuala ya mazingira na Afrika wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa
Mataifa ya Afrika Mashariki yamekekuwa yakikabiliana na makundi ya nzige tangu mwaka wa 2020. Kwa kile kinachotambuliwa kama mkurupuko mbaya kuwahi kutokea katika eneo hilo kwa miongo kadhaa, Shirika la Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa linatoa onyo kuwa kuongezeka kwa idadi ya nzige wa jangwani ni tishio kubwa kwa upatikanaji wa chakula cha kutosha na kwa maisha ya watu katika eneo la Pembe ya Afrika.
Kutokana na taarifa za shirika hilo zilizotolewa hivi karibuni kuhusiana na kuongezeka kwa nzige, hali iliopo inaweza kuwa mbaya zaidi wanapoendelea kuzaana na kuzidisha madhara katika nchi za Ethiopia, Kenya na Somalia. Pia, kuna uwezekano wa kusambaa katika maeneo mengine.
Tulifanya mahojiano na Richard Munang, mtaalamu wa masuala ya mazingira na Afrika wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ili kufahamu uhusiano uliopo kati ya vigezo vya kimazingira, mabadiliko ya tabianchi na kujitokeza kwa nzige.
Kuna uhusiano upi kati ya nzige na mabadiliko ya tabianchi?
Wakati kumetulia—kipindi cha mafichoni—mara nyingi, nzige wa jangwani huwa katika maeneo kame na majangwani barani Afrika, Maeneo ya Asia Mashariki na Kusini Mashariki mwa Asia. Haya ni maeneo ambayo hushuhudia chini ya milimita 200 za mvua kila mwaka. Katika hali ya kawaida, idadi ya nzige hupungua kupitia kufa wenyewe au kwa kuhama.
Hata hivyo, miaka mitano iliyopita imekuwa na joto jingi kushinda miaka mingine yeyote tangu wakati wa mapinduzi ya viwanda na tangu mwaka wa 2009. Tafiti zimeonyesha uhusiano kati ya mabadiliko ya tabianchi na makundi makubwa ya nzige waharibifu—nchi 20 kati ya nchi zinazoshuhudia ongezeko la joto kwa kasi duniani zinapatikana barani Afrika. Hali ya anga pia huvutia kuongezeka kwa nzige. Kuongezeka kwa mvua kuliko kiwango cha kawaida kulikoshuhudiwa kwenye Pembe ya Afrika tangu Oktoba hadi Desemba mwaka wa 2019 ilikuwa asilimia 400 zaidi ya kiwango cha kawaida cha mvua. Mvua hii isiyokuwa ya kawaida ilisababishwa na mabadiliko kwa Bahari Hindi, dhana inayotokana na mabadiliko ya tabianchi.
Je, nchi na watu binafsi wanaweza kijitayarisha vipi?
Ijapokuwa mabadiliko ya tabianchi hushuhudiwa kote ulimwenguni, Afrika ina uwezekano mkubwa wa kuathiriwa. Hali hii inayotokana kimsingi na kiwango duni cha maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi. Watu wanaoishi maisha ya ufukara wana uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi kwa sababu hawana rasilimali za kukabiliana kwa kasi na madhara yake. Katika hali kama hii, nzige wa maeneo ya jangwani huangamiza mimea mashambani kabla ya mavuno. Hali inayopunguza chakula cha mifugo na wanyamapori na hivyo kuathiri maisha ya binadamu.
Kwa kutumia suluhu zinazojali mazingira kama vile kuwezesha watu wengi kutumia mitambo inayotegemea jua kukausha mazao yao ya kilimo kunaweza kusababishia wakulima faida zaidi ya mara 30 kwa kuweza kuhifadhi mazao yao na kuwawezesha kuyauza wakati yasipopatikana kwa urahisi. Pia, inaweza ibua fursa iwapo wahusika watajitengenezea mitambo inayotumia jua. Kufanya hivi ni muhimu ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika jamii zinazoathiriwa pakubwa barani.
Je, nzige wanaweza kudhibitiwa vipi?
Ili kukabiliana na mawimbi ya nzige wa maeneo ya jangwani kemikali za oganofosfeti hutumika kupitia vinyunyuzio vilivyofungwa kwenye magari au kwa kunyuzia angani. Pia, ijapokuwa si maarufu, wanaweza kunyunyiziwa kwa kutumia shanta na vinyunyuziaji vinavyoshikwa mkononi.
Utafiti wa kina unaendelea kufanywa kuhusiana na udhibiti wa kibayolojia na mbinu nyinginezo zisizotumia kemikali. Zaidi, watafiti wanatilia maanani uchunguzi wa pathojeni na wa vifaa vinavyoweza kudhibiti nzige. Njia ya kudhibiti nzige kwa kutumia viumbe vamizi na vimelea imefeli kwa sababu nzige wanaweza kuhama na kuepukana na adui wanaojitokeza. Hata kama mara nyingi watu na ndege hula nzige, hali hii haiwezi kupunguza idadi ya nzige walioenea.
Umoja wa Mataifa hufanya nini kukabiliana na nzige?
Umoja wa Mataifa hutumia mbinu anwai kukabiliana na nzige. Ijapokuwa upatatikanaji wa chakula cha kutosha utaathiriwa, mabadiliko ya tabianchi huchochea kutokea kwa hali hii.
Mojawapo wa kazi za UNEP ni kusambaza taarifa zinazowafikia za kisayansi kuhusiana na tabianchi na mielekeo yake ili kuwezesha uundaji wa sera jumuishi na kuhakikisha sekta husika zinachukua hatua za kuwezesha ustahimilivu.
Kazi ya Shirika la Metolojia Duniani ni kutabiri na kutangaza madaliko ya hali ya hewa yanayojitokeza yanayoweza kusababisha uvamizi wa nzige.
Ijapokuwa tangu jadi kemikali zimetumiwa kudhibiti nzige athari ya kemikali hizi kwa mazingira na kwa mifumo mingine mikuu ya ekolojia inayowezesha kuwepo kwa chakula cha kutosha—kama vile nyuki na wadudu wengineo, ambao mbali na kuchavusha asilimia 70 ya chakula chetu pia wanaathiri afya zetu— ni suala lisiloweza kupuuzwa. Kazi ya Shirika la Chakula Duniani ni kuorodhesha madhara yoyote yanayoweza kutokea kwa kutumia ania mbalimbali za kemikali ili kuwezesha serikali kuwekeza kwa zile zisizo na madhara.
Mojawapo wa kazi ya Shirika Kilimo na Chakula ni kutoa taarifa za jumla kuhusu uvamizi wa nzige na kutoa onyo mapema na kutabiri kuhusu nchi zinazoweza kuvamiwa. Shirika hilo hutoa taarifa kuhusu nzige wa maeneo ya jangwa. Kwa kuongezea, kuwezesha jamii kupata teknolojia iliyo na manufaa mengi kama vile mashine ya kukaushia yanayotumia jua—ambazo pia ni hatua za kujali mazingira—huwasaidia kutunza mazao yao. Hali hii inawezesha kuvuna mapema kabla ya kuvamiwa na nzige ili kuepusha mazao yao kuvamia zaidi.