30 Jul 2020 Tukio Kutumia mazingira kushughulikia tabianchi

Mbali na Utalii: kuwekeza kwenye jamii za kiasili ili kutunza maeneo ya wanyamapori barani Afrika

https://www.youtube.com/watch?v=ttfIyL2w6qI&feature=youtu.be

 

Kwa kipindi cha miaka kumi, Dixon Parmuya amewaelekeza watalii porini katika Mbuga ya Kitaifa ya Amboseli, Kusini mwa Kenya. Lakini tangu janga la COVID-19 lilipoingia nchini Kenya katikati ya mwezi wa Machi, sekta ya utalii nchini humo imedidimia, na kuwaacha wenyeji wengi bila kazi na wanyama bila ulinzi.

Janga la virusi vya korona lilisababishwa kile kinachorejelewa na wataalamu kama uwezekano wa kuwa na mzozo wa kuhifadhi nchini Kenya, nchi iliyo na wanyama wa kipekee barani Afrika. Progamu nyingi nchini Kenya za kulinda wanyamapori hufadhiliwa moja kwa moja na dola zinazotolewa na watalii, na wakati ambapo idadi ya wageni imepungua, pesa za kutumiwa kwenye hifadhi zinaendelea kuisha, wataalamu wasema. Kuna hofu ya kuongezeka kwa uwindaji haramu, na kuhatarisha usalama wa wanyamapori.

"Kama hakuna utalii, hakuwezi kuwa na hifadhi," asema Parmuya.

Lakini janga lilopo linataka nchi kupadisha mwenendo huo.

A masai
Dixon Parmuya. Picha na UNEP / Georgina Smith

"Utalii hauwezi kutegemewa," anasema Doreen Robinson, Mkuu wa Wanyamapori katika Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). "Ni sharti tuwe wabunifu zaidi ili kupata fedha zinazoweza kunufaisha wenyeji na kutunza malighafi."

Barani Afrika, UNEP inashirikiana na serikali na wabia ili kuhimiza kuwepo na uchimi unaotegemea wanyamapori – ambapo jamii za wenyeji zitakuwa mstari mbele kutunza maeneo ya wanyamapori wanayokalia, kwa manufaa kwa wanyama na kwa binadamu. Hii inahakikisha kuwa mbali na utalii kuna uwekezaji usiochafua mazingira kwenye maeneo yanayokaliwa na wanyamapori, kama vile kutumia malighafi kuzalisha bidhaa kwa njia endelevu. 

"Ni sharti tuhakikishe ya kwamba fedha zinaekezwa tena katika maeneo yaliyohifadhiwa, na kuwa manufaa yanayopatikana yanagawiwa jamii zinazotunza bayoanuai na wanyamapori. Hii ni kwa sababu jamii hizi zitawezesha kuwepo na hifadhi za kudumu kwa njia endelevu nchini Kenya," anasema Robinson.

Ranger Purity Amleset
Purity Amleset. Picha na UNEP / Georgina Smith

Purity Amleset anakubaliana na hayo. Yeye ni mmoja wa kikosi cha askaripori kinachojumuisha tu wanawake kinachofanya kazi na Mfuko wa Kimataifa wa Masilahi ya Wanyama kinachohamasisha kuhusu umuhimu wa wanyamapori kwa uchumi wa Kenya na utambulisho wake.

"Kama askaripori, ninaweka mazingira mazuri kati ya wanyamapori na jamii." Natoka kwenye hiyo jamii, na kwa hivyo, wananielewa vyema ninapowaelezea kuhusu umuhimu wa wanyamapori," anasema.

Maadhimisho ya Askaripori Duniani hutokea tarehe 31 Julai ya kila mwaka kujivunia asikaripori kote ulimwenguni wanaohatarisha maisha yao kila siku kwa kuwa mstari mbele katika shughuli za uhifadhi.

Rangers and Maasai
Kikosi cha askaripori cha Lioness  kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Masilahi ya Wanyama(IFAW) kikizungumza na jamii katika mbuga ya Kitaifa ya Amboseli. Picha na UNEP / Georgina Smith

 

covid-19 response logo