1. Sayari inayotegemea nishati isiyochafua mazingira| Mkataba wa Paris wa Mazingira
Tunahitaji nishati kila siku tunayoishi, ila sayari yetu inaendelea kuwa na joto zaidi kwa sababu umeme wetu mwingi hutokana na fueli ya visukuku. Ila, hatuhitaji kuchagua kati ya kutumia nishati na kutunza sayari. Mshindi wa Tuzo la Umoja wa Mataifa la Vijana Bingwa Duniani Nzambi Matee anaonyesha jinsi tunavyoweza kujenga dunia ambayo kila nafasi ya kazi inategemea nishati jadidifu isiyochafua mazingira. Safari yetu kuelekea hatima hii ni Mkataba wa Paris wa Mazingira.
2. 2. Miji Safi | Mkataba wa Paris wa Mazingira
Tuna uwezo wa kufahamu jinsi ya kubadili miji yetu iwe na kijani, na usafiri usiochafua mazingira na majengo yanayotumia nishati vizuri. Mshindi wa Tuzo la Umoja wa Mataifa la Vijana Bingwa Duniani Nzambi Matee anaeleza jinsi tunavyoweza kufikia haya, kwa kuongozwa naMkataba wa Paris wa Mazingira. Nzambi ni mhandisi aliyeanzisha kampuni yake mjini Nairobi, nchini Kenya, inayotengeneza matofali kutoka kwa taka ya plastiki. Hatima ya miji yetu inaweza kuwa nzuri na isyochafua mazingira. Hii ni ya pili kwa mfululizo wa video zinazotoa maelezo chini ya "Within Our Grasp".