Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Inger Andersen, Hivi majuzi alitembelea Malawi,ambapo miezi kadhaa baadaye, uharibifu wa Kimbunga Freddy unaendelea kudhihirika.
Mojawapo ya dhoruba mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kusini mwa ikweta, kimbunga hicho kilidhuru maeneo makubwa ya kusini mwa Afrika kwa wiki tano katika miezi ya Februari na Machi. Hata Malawi, nchi iliyozungukwa na nchi kavu haikuachwa nyuma. Katika sehemu kubwa ya nchi, mafuriko na maporomoko ya udongo yaliharibu nyumba, barabara, shule, vituo vya afya, madaraja, vyanzo vya maji, mimea na mifumo ya unyunyuziaji mimea maji.
Kote ulimwenguni, dhoruba zinaendelea thabiti na kutokea mara kwa mara, hali inayowafanya wanasayansi kuyahusisha na mabadiliko ya tabianchi. Katika maeneo mengi, ikijumuisha Malawi, hali ya mafuriko kutokana na mvua nyingi huwa mbaya zaidi kutokana na ukataji miti, unaoondoa mimea juu ya ardhi, na kupelekea maporomokoya ardhi yanayopelekea uaribifu.
Wakati wa ziara zake, Andersen alisema dunia ni sharti iimarishe juhudi zake ili kusaidia mataifa yanayoendelea, kama vile Malawi, kukabiliana na hali y hewa inayobadilika.
"Haikubaliki kuwa nchi anbazo hazijachangia mno katika mabadiliko ya tabianchi huathirika zaidi," alisema.
UNEP inafanya kazi na serikali za eneo, taasisi nyingine za Umoja wa Mataifa na mashirika ya wahisani kutafuta masuluhisho yanayotokana na mazingira ya kukabiliana na mafuriko na maporomoko ya ardhi.