Photo by Xinhua via AFP
13 Aug 2024 Tukio Kushughulikia Mazingira

Juhudi za kusafisha mojawapo ya barabara chafu zaidi za usafiri barani Afrika

Photo by Xinhua via AFP

Wakati dereva wa lori Salim Awadh aliposafiri hadi Mombasa, nchini Kenya mwaka wa 2021 kupokea mafunzo kuhusu udereva unaotumia mafuta vizuru, alikuwa akisafirisha mizigo Afrika Mashariki kote kwa takriban miongo miwili. 

Bado, kozi hiyo ilimfanya mtu huyu wa miaka 53 kupata maono, kwa kuwa yeye husafiri mara nyingi katika barabara ya Ukanda wa Kaskazini, msururu wa barabara kuu zinazopitia nchi sita.   

Mjini Mombasa, mmojawapo wa walimu alimwonyesha Awadh jinsi ya kuokoa mafuta kwa kutumia kasi ileile, kwa kutumia gia ya juu zaidi iwezekanavyo na kuepuka kuongeza kasi pasipohitajika.   

Leo, Awadh anasema kuwa yeye hutumia mafuta yaliyopungua kwa takriban asilimia 20 ikilinganishwa na alivyokuwa akitumia hapo awali, na ameokoa pesa na kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa bomba lililoko kwa lori lake la magurudumu 22. 

"Ujuzi wetu wa kuendesha magari unaendelea kuboreka jambo ambalo hutuongezea kipato," anasema Awadh.   

A man driving a truck.
Malori hadi 3,000 hupitia Ukanda wa Kaskazini kila siku, na kuufanya kuwa sehemu kuu ya uchafuzi wa mazingira na uzalishaji wa gesi ya ukaa. Picha na AFP/Brian Ongoro

The driving workshop Awadh attended was part of a larger effort, backed by the United Nations Environment Programme (UNEP) and Warsha ya kuendesha magari ambayo Awadh alihudhuria ilikuwa sehemu ya juhudi kubwa zaidi, zilizoungwa mkono na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Muungano wa Mazingira na Hewa Safi unaoungwa mkono na UNEP ili kuboresha matumizi bora ya mafuta kwa Ukanda wa Kaskazini, mojawapo ya barabara za usafiri zilizo na shughuli nyingi zaidi barani Afrika. Waangalizi wanasema upunguaji huo ni muhimu katika kupunguza uchafuzi wa hewa na uzalishaji wa gesi ya ukaa- na hatimaye kutoa fursa ya usafiri wa umeme usiozalisha hewa chafu.  

"Kwa kubadilisha Ukanda wa Kaskazini, tunaweza kuonyesha kwamba usafiri barani Afrika hauhitaji kugharamu mazingira na afya ya binadamu," anasema Sheila Aggarwal-Khan, Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda na Uchumi ya UNEP.  "Lakini zaidi ya hayo, kazi hii inaweza kutumika kama msingi wa mustakabali wa usafiri usiochafua mazingira, mabadiliko yanayopaswa kufanywa na ulimwengu ili kudhibiti majanga yanayoongezeka ya mabadiliko ya tabianchi na uchafuzi.” 

Kiungo muhimu  

Ukanda wa Kaskazini ni mkusanyo wa barabara, reli, mabomba na njia za kupitia majini zinazounganisha nchi nyingi zisizo na bandari za Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na bandari ya Mombasa nchini Kenya. Mizigo inayosafirishwa barabarani huchangia kiwango kikubwa cha trafiki. Kati ya malori 2,000 na 3,000 hupitia barabara hii kila siku, huku yakiwa yamebeba kila kitu kuanzia kwa chakula hadi kwa vifaa. 

Hali hii imeifanya kuchangia pakubwa kwa uchafuzi wa hewa, anasema dereva wa lori Moses Radier, ambaye husafirisha mizigo kati ya Rwanda na Kenya. Madereva wengi, anasema, huugua magonjwa ya mfumo wa kupumulia na hukabiliwa na kikohozi cha mara kwa mara, ambapo mara nyingi hali huwa mbaya zaidi kutokana na vumbi kutoka kwa barabara zisizo na lami.  

Utoaji wa hewa chafu kwenye mabomba ya magari pia huwaumiza watu wanaoishi kando ya ukanda huo, unaopitia mamia ya vijiji na miji kwa barabara ya mzunguko kutoka Kisangani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hadi Mombasa. 

Trucks rumble along a road overlooking a deep valley
Juhudi zinazoenea, zinazoungwa mkono kwa kiwango fulani na UNEP, zinalenga kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa na kupunguza uchafuzi wa hewa kwa Ukanda wa Kaskazini, mojawapo ya barabara za usafiri zilizo na shughuli nyingi zaidi barani Afrika. Picha na AFP/Tony Karumba

Ili kukabiliana na athari za uchafuzi, Mamlaka ya Uratibu wa Usafiri na Uchukuzi wa Ukanda wa Kaskazini - taasisi ya serikali mbalimbali - imezindua mikakati miwili inayojulikana kama "usafiri pasi na kuchafua mazingirai" na msaada kutoka kwa UNEP na Muungano wa Mazingira na Hewa Safi. Wa hivi karibuni uliidhinishwa na mawaziri wa kitaifa mwezi wa Juni.  Unalenga kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa vichafuzi vitatu vya kawaida - chembechembe, kaboni nyeusi na nitrojeni oksidi - kwa asilimia 12 ndani ya muongo huu. Vichafuzi hivi  vimehusishwa na magonjwa ya moyo, kiharusi, pumu na matatizo mengine kadhaa ya afya.   

Mkakati huu pia unalenga kupunguza uzalishaji wa kaboni dioksidi, gesi ya ukaa inayochangia mabadiliko ya tabianchi kwa asilimia 10. Katika mwaka wa 2018, magari katika ukanda huo yalizalisha kaboni dioksidi zaidi ya tani 1.7.   

"Kufikia malengo ya Mkakati wa 2030 wa Usafiri Pasipo na Uchafuzi mbali na kurandana na malengo ya Mkataba wa Paris pia kuhakikisha mfumo wa usafirishaji wa mizigo katika ukanda huu unasalia kuwa imara na kubadilika kwa kutegemea mabadiliko duniani," anasema Omae Nyarandi, Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Uratibu wa Usafiri na Uchukuzi wa Ukanda wa Kaskazini.  

Kote duniani, sekta ya uchukuzi inawajibikia asilimia 15 ya uzalishaji wa kaboni dioksidi, gesi ya ukaa inayochangia mabadiliko ya tabianchi. Uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa sekta hii unakua kwa kasi zaidi kuliko sekta nyingine yoyote na unanuiwa  kuongezeka maradufu kufikia mwaka wa 2050, hasa kutokana na ongezeko kutoka kwa nchi zinazoendelea.   

Kudhibiti uzalishaji wa hewa chafu za usafiri kunachukuliwa kuwa muhimu kukabiliana na joto ilnaloongezeka kwa kasi duniani, ambalo lilitumia mwaka jana kuvunja rekodi. Kuanza kutumia magari ya umeme, kukuza matumizi mapana ya usafiri wa umma na kupanga miji vizuri zaidi ili kupunguza hitaji la usafiri, miongoni mwa sera nyinginezo, kunaweza kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kutokana na usafiri kwa zaidi kwa asilimia 50, kama ilivyopata UNEP.  

Mapendekezo ya sera 

Mkakati wa usafirishaji wa mizigo wa Ukanda wa Kaskazini unapendekeza nchi kuanzisha viwango vya matumizi bora ya mafuta, kuzuia uagizaji wa malori kuukuu, na mabovu, kuwekeza katika njia za usafiri zisizochafua mazingira kama vile reli, kutumia magari ya umeme na kuboresha teknolojia ili kuboresha matumizi ya mafuta kwa malori.    

Pia madereva 2,000 wanahitaji kupewa mafunzo ya jinsi ya kubeba mizigo vizuri zaidi. Uchanganuzi uligundua lori la masafa marefu likiendeshwa kwa kilomita 2,500 kwa mwezi linaweza kuokoa hadi shilingi 30,000 za Kenya (US$230) kwa gharama za mafuta yakiendesha kwa njia bora.  

"[Hali hii] itaboresha maisha ya madereva kifedha, na kuwaruhusu kutunza familia zao vyema," anasema Newton Wang'oo, Mkurugenzi wa One-to-One Logistics nchini Kenya, shirika linalotoa masuluhisho ya uchukuzi katika ukanda huo.    

The Northern Corridor connects several landlocked East African countries to the Kenyan port city of Mombasa.
Ukanda wa Kaskazini unaunganisha nchi kadhaa za Afrika Mashariki zisizo na bandari na mji wa bandari wa Mombasa nchini Kenya  Picha na Xinhua kupitia AFP   

In June 2024, ministers from the corridor’s six countries called for the implementation of the 2030 strategy to be fast tracked. Katika Mwezi Juni mwaka wa 2024, mawaziri kutoka nchi sita za ukanda huu walitaka utekelezaji wa mkakati wa 2030 ufuatiliwe haraka. Wakati uo huo, mataifa yanalenga kuwezesha barabara ya urefu wa kilomita 2,000 kustahimili athari za mabadiliko ya tabianchi, ikijumuisha mafuriko. 

Nchi zilizo kwenye ukanda huu zimejitolea kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa katika sekta ya uchukuzi, ikiwa ni pamoja na wa mizigo, kupitia  michango yao iliyoamuliwa kitaifa, mfululizo wa ahadi zinazohusiana na tabianchi. Awamu mpya ya michango hii inatarajiwa katika mwaka wa 2025.  

"Ahadi hizo lazima zifanyiwe kazi na kuwa sheria na kanuni thabiti ambazo zitabadilisha na kutoa motisha kwa sekta ya uchukuzi," anasema Aggarwal-Khan.   

Kusafiri pasipo na kuchafua Ukanda wa Kaskazini, anaongeza, ni sharti iwe sehemu ya jitihada kuu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kupunguza uchafuzi wa hewa, ambao unahusishwa na  vifo milioni 1.1 kila mwaka barani Afrika. 

Madereva wa malori, kama vile Moses Radier, wana matumaini makubwa ya kukomesha uchafuzi katika ukanda huo. “Walioko katika sekta ya uchukuzi wataokoa fedha, uchafuzi utapungua, afya zetu zitaimarika na tutakuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi,” anasema. 

 

Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na anga za bluu 

Maadhimisho  ya Siku ya Kimataifa ya Hewa Safi ili kuwa na angaa za bluu, ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 7 Septemba na kuendeshwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), huhamasisha kuhusu umuhimu wa hewa safi kwa afya, kwa utendakazi, kwa uchumi na kwa mazingira.  Kaulimbiu ya mwaka huu "Wekeza kwa #HewaSafiSasa" inaonyesha ya kuwekeza kwa hewa safi manufaa kwa chumi, mazingira na afya.  

Mpango wa UNEP wa Mafuta na Magari Yasiyochafua Mazingira  

Mpango huu unashirikiana na mashirika ya umma na ya kibinafsi kuwezesha mabadiliko ya kutumia usafiri wa barabarani unaozalisha kiwango kidogo cha hewa ya ukaa. Ili kufikia hili, unapigania kuwekwa kwa viwango vya uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa magari na kuhimiza matumizi ya teknolojia isiochafua mazingira. Kuanzia tarehe 25 hadi 26 Machi mwaka wa 2024, UNEP na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi nchini Uganda waliandaa warsha ya siku mbili ya kueneza Mkakati wa 2030 wa Usafiri Pasipo na Uchafuzi kwa Ukanda wa Kaskazini kutafuta fursa za usafiri usiochafua mazingira.  

 Masuluhisho ya Kisekta  kwa janga la mabadiliko ya tabianchi   

UNEP iko mstari mbele kuunga mkono lengo la  Mkataba wa Paris la kudhibiti kiwango cha joto duniani kisizidi nyuzijoto 2, na kulenga nyuzijoto 1.5, ikilinganishwa na viwango vya kabla ya viwanda. Ili kufikia lengo hili, UNEP imeunda Masuluhisho ya Kisekta, mwongozo wa kupunguza uzalishaji wa hewa chafu katika sekta mbalimbalikwa kuzingatia ahadi katika Mkataba wa Paris ili kuwezesha kuwa na mazingira thabiti. Sekta zilizoainishwa ni: mifumo ya nishati, viwanda; AFOLU (kilimo, misitu na matumizi mengine ya ardhi, uchukuzi, na ujenzi.