Kikao cha tano cha Mkutano wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-5.2) kitaendeshwa mtandaoni na mjini Nairobi kuanzia tarehe 28 Februari hadi tarehe 2 Machi 2022.
Kaulimbiu kuu ya UNEA-5 ni “Kuimarisha Juhudi za Kushughulikia Mazingira Ili Kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ”. Hali inayoangazia wajibu muhimu unaotekelezwa na asili kwa maisha yetu na kwa maendeleo endelevu katika jamii, uchumi na mazingira.
Punde tu baada ya UNEA-5.2, Baraza hili litaendesha Kikao Maalum cha Baraza tarehe 3 hadi 4 Machi 2022, ambacho kitatumiwa kuendesha maadhimisho ya 50 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa katika Mwaka wa 1972 (UNEP@50). Endelea kutufuatilia!
Hapa utapata kila kitu unachohitaji kujua kuhusu UNEA-5 na UNEP@50 pamoja na linki za vikao vinavyoendelea moja kwa moja, ripoti mpya na mijadala muhimu inapotokea. Endelea kufuatilia!