15 July 2024 Ripoti

Ripoti ya mtazamo wa kimataifa kuhusu afya ya sayari na ustawi wa binadamu

Waandishi: UNEP
Cover

Ripoti hiyo itapatikana tarehe 15 Julai mwaka wa 2024

Ili kusaidia kukabiliana na kutokuwa na uhakika na mabadiliko ya sasa na katika siku zujazo, huku ikitekeleza wajibu wake vyema, UNEP imekuwa ikitekeleza mbinu ya kitaasisi ya kubashiri mkakati na kuangazia mambo kwa lengo la kuendeleza utamaduni unaoweza kutabirika na unaozingatia siku zijazo. 

Hii inaakisi kuongezeka kwa nia na mahitaji ya ubashiri ambao unaimarishwa pia na ajenda ya mageuzi ya Umoja wa Mataifa na ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu 'Ajenda Yetu ya Pamoja', ambayo inatoa wito kwa mashirika yote ya Umoja wa Mataifa, pamoja na nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa, kufanya utabiri wa kina na kutumia maarifa yaliyopatikana kushughulikia hatari za kimfumo za kimataifa.

Mchakato huu umepelekea kuandaliwa kwa ripoti ya sasa "Kuzingatia Maeneo Mapya - Ripoti ya Mtazamo wa Kimataifa kuhusu Afya ya Sayari na Ustawi wa Binadamu", iliyotolewa na UNEP kwa ushirikiano na Baraza la Kimataifa la Sayansi. Ripoti hiyo inatoa wito kwa ulimwengu kuzingatia na kushughulikia changamoto mbalimbali zinazojitokeza ambazo zinaweza kutatiza afya ya sayari na ustawi. Inaangazia kuhusu mabadiliko manane muhimu ya kimataifa ambayo yanaongeza kasi ya changamoto za aina tatu duniani tatu za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na wa mazingira, na uchafuzi na taka.

Ishara kumi na nane za mabadiliko - zilizotambuliwa na mamia ya wataalam wa kimataifa na kusambazwa kupitia mashauriano ya kikanda na washikadau ambayo yalijumuisha vijana - inatoa muhtasari wa mambo yanayoweza kutokea, mazuri na mabaya, ambao ulimwengu unahitaji kuendelea kuyafuatilia.  Ripoti hii inaeleza jinsi ya kuunda mazingira mema ili kufanya maamuzi bora kwa kuunda mkataba mpya wa kijamii, kukumbatia uongozi unaoweza kubadilikabadilika kutegemea hali, na kuongeza data na maarifa yanayohusiana.

Ripoti hii ni ukumbusho wa maingiliano na udhaifu wa mifumo yetu katika Karne ya 21 na inaonya kuwa kuweka mbele manufaa ya muda mfupi kuliko hatua za kubashiri na kujiandaa kunahatarisha ustawi wa muda mrefu na afya ya sayari. Hata hivyo, pia inaangazia uwezo mkubwa na werevu wa binadamu ambao unaweza kutumiwa katika ari ya kutambia na kushirikiana kutoa masuluhisho kwa janga la aina tatu.

Matokeo ya ripoti hii yatajumuishwa katika mpango mkakati wa UNEP, ambao unaweza kuathiri MTS ijayo ya UNEP, na kuwasilisha fursa ya kufikiria kupanua programu katika maeneo kama akili unde, teknolojia mpya, na roboti katika kilimo, na kupelekea majadiliano kuhusu kiwango cha kushauriana kuhusu mambo haya. Haya hatimaye yatasaidia UNEP kuchukua msimamo na kuboresha zana zake ili kupata ufanisi na kupunguza gharama. 

Zaidi ya hayo, ripoti hii itatumika kama mchango wa UNEP kwa Mkutano wa Kilele wa Mstakabali.  Ingawa haitarajiwi kuathiri kwa kiasi kikubwa Mkutano wa Kilele wa Mstakabali, itatumika kutoa michango katika majadiliano na hafla za maandalizi, ikijumuisha Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu, tunapoelekea Mkutano wa Kilele wa Mstakabali kwa sababu inahusiana na vipengele vya mazingira.