Baadhi ya jumbe muhimu kutoka kwenye ripoti hiyo
1. Ripoti ya sita ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ya Hali ya Mazingira Duniani (GEO-6) ni ya kina zaidi kuhusu mazingira duniani tangu mwaka wa 2012. Inaonyesha kuwa hali ya jumla ya mazingira duniani inazidi kuzorota na fursa ya kushughulikia hali hiyo inaendelea kupungua.
2. GEO-6 inaonyesha kuwa mazingira ni nguzo na msingi wa ustawi wa kiuchumi, afya ya binadamu na ustawi. Inaangazia changamoto kuu kwa Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu: kwamba hakuna mtu anayepaswa kuachwa nyuma, na kwamba kila mtu anapaswa kuishi maisha yenye afya, mazuri kwa manufaa kamili kwa wote, kwa vizazi vilivyopo na vizazi vijavyo.
3. Mifumo isiyo endelevu ya uzalishaji na ruwaza na mienendo isiyoendelevu na ukosefu wa usawa vikijumuishwa na ongezeko la matumizi ya rasilimali kutokana na ongezeko la watu, ni tishio kwa sayari bora inayohitajika ili kuwa na maendeleo endelevu. Mienendo hiyo inasababisha kuzorota kwa hali ya sayari kwa viwango ambavyo havijawahi kushuhudiwa, kukiwa na madhara mbaya zaidi, haswa kwa watu maskini na maeneo maskini.
4. Zaidi ya hayo, ulimwengu hauelekei kufikia vipengele vya mazingira vya Malengo ya Maendeleo Endelevu au malengo mengine ya mazingira yaliyokubaliwa duniani kufikia mwaka wa 2030; wala hauelekei kufikia uendelevu wa muda mrefu kufikia mwaka wa 2050. Hatua za dharura na ushirikiano wa kimataifa ulioimarishwa
vinahitajika kwa dharura ili kubadili mielekeo hiyo ghasi na kurejesha ubora wa sayari na afya ya binadamu.
5. Uzalishaji wa gesi ya ukaa zamani na za sasa tayari umepelekea dunia kushuhudia kipindi kirefu cha mabadiliko ya tabianchi huku madhara anuai yakitokea kwa mazingira na kwa jamii nzima.