Publication

Mazingira ni Nguzo ya Maendeleo Endelevu

24 January 2022
Jalada

Kikao cha Tano cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-5) ni fursa ya kuimarisha, kuboresha na kuchombea athari zinazohusiana na juhudi za kimataifa za kushughulikia mazingira ikijumuisha kuhusu bayoanuai, hali ya hewa, mifumo ya chakula na uchafuzi – na pia ni mwanzo wa kipindi cha kutafakari na maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa UNEP.

Makala haya yameandaliwa ili kusaidia Nchi Wanachama na wawakilishi wengineo wa ngazi ya juu ikijumuisha  kutoka viwandani na mashirika ya uraia, kujiandaa kwa mkutano ujao wa UNEA-5, utakaoandaliwa mjini Nairobi,  nchini Kenya, kuanzia tarehe 28 Februari hadi tarehe2 Machi 2022 chini ya kaulimbiu “Kuimarisha Juhudi za Kushughulikia Mazingira ili Kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.” Ni wito wa kuchukua hatua chini ya kila  vipengele vinne vya UNEA na fursa ya kuchukua hatua- kwa manufaa ya watu na sayari .