Publication

Vipaumbele vya Kimkakati vya Maji Safi vya miaka ya 2022 hadi 2025

22 March 2022
Report cover

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) limetoa stakabadhi mpya ya kimkakati inayoelezea vipaumbele vyake vinavyohusiana na maji safi ili kutekeleza Mkakati wa Muda wa Kati (MTS) wa UNEP, 2022-2025. Haya yanalenga kuchochea uelewa wa haraka, vipaumbele na hatua za maji zinazohitaji kuchukuliwa duniani kote.

Makala yaliyotolewa na Kikundi cha Maji cha Divisheni Mbalimbali, jamii ya utendajikazi ndani ya UNEP, makala haya yanaelezea vipi na jinsi masuala ya maji safi yanavyosaidia kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu yanayohusiana na maji na kushughulikia majanga matatu yanayoingiliana duniani katika MTS:

• Mabadiliko ya tabianchi
• Uharibifu wa mazingira na uharibifu wa bayoanuai
• Uchafuzi na taka

Madhara ya majanga haya yote matatu duniani huathiri moja kwa moja, na katika hali zingine kwa njia mbaya, vyanzo vya maji safi, ambavyo ni muhimu kwa maisha, riziki na afya ya watu, uchumi na sayari. 

Wakati uo huo, vikitunzwa vyema, vyanzo vya maji safi ni washirika wakuu katika kupambana na majanga haya yote matatu. Vyanzo vya maji safi vinaweza kusaidia kulinda na kurejesha bayoanuai, kupunguza uchafuzi kupitia uchujaji na usafishaji wa maji, na kuchangia kwa uthabiti wa mazingira kwa kutoa manufaa ya kukabiliana na kushughulikia hali hii. 

Kwa kuwa maji yanatishiwa, kuna hitaji la lazima la kuchukua hatua.  Pamoja na washirika, UNEP inatafuta kuwezesha maendeleo yanayoweza kupimika na makubwa kuhusiana na masuala ya maji safi katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa.

Mada