Makala haya sanisi yanawasilisha ujumbe kuhusu jinsi ambavyo mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na uchafuzi vinavyoweza kushughulikiwa kwa pamoja chini ya Malengo ya Maendeleo Endelevu. Ripoti hiyo inalenga kfanya maarifa ya kisayansi yaliyopo kuwa ujumbe halisi, wa wazi, unaoeleweka kwa urahisi ili dunia iyatambue na kuyafuatilia. Inaanza kwa kueleza hali ya sasa ya dunia na jinsi ambavyo shughuli za binadamu zimesababisha madhara kwa mazingira, kwa kuzungumzia mambo halisi na kuonyesha yanavyoingiliana ikijumuisha kutumia infografiki za kisasa. Kutokana na hali hii, ripoti hii inaonyesha mabadiliko yanayohitajika ili kupunguza mapengo yaliyopo kati ya hatua zilizochukuliwa na zile zinazohitajika ili kufikia malengo endelevu. Uchanganuzi huu unazingatia hali halisi ya sasa ya uchumi, ya jamii na ya ya ekolojia kwa kuzingatia uchumi na ajenda 2030 ya Maendeleo Endelevu. Kupitia usanishaji wa matokeo ya utafiti wa hivi karibuni kutokana na utafiti wa kimataifa kuhusiana na mazingira, ripoti hiyo inaelezea kuhusu hali ya sasa ya masuala yanayohitaji kushughulikiwa kwa dharura na kutoa fursa ya kuyatatua.
Muungano wa Ulaya ni mfadhili mwenza wa mradi huu