Kijitabu hiki ni mhutasari kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa-sisi ni nani, kuhusu kazi tunayoifanya, mbona tunaifanya na jinsi tunavyoifanya.
Tangu mwaka wa 1972, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa limefanya kazi kazi kama mhamasishaji mkuu wa masuala ya mazingira. Lengo letu ni kuelimisha, kuwezesha na kushawishi mataifa na watu binafsi kuboresha hali yao ya maisha- bila kuhatarisha ya vizazi vijavyo. Tunafanya kazi chini ya Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka wa 2030 kwa kubainisha na kushughulikia masuala nyeti yanayoathiri mazingira katika kipindi hiki tunachoishi.
Chapisho hili linaeleza kuhusu kazi tunayoifanya kwa kutolea mifano maeneo mbalimbali ambayo huwa tunafanya kazi, na kuonyesha yale ambayo tumefanikiwa kutimiza kwa ushirikiano na wabia wetu.
Kazi yetu hufanikishwa na wabia wanaoifadhili na kuhamasisha watu kuihusu. Chapisho hili linaangazia umuhimu wa kuwa na kiini cha rasilimali zinazoweza kubadilikaza ili kuwezesha ufadhili wa kazi yetu; jinsi suala hili lilivyo muhimu kwa kazi yetu na hutuwezesha kuajiri watu waliohitimu na wataalamu kufanya kazi tuliopewa na Nchi Wanachama 193.