08 November 2023 Ripoti

Ripoti ya Pengo la Juhudi za Kukabiliana na Gesi Chafu mwaka wa 2023:

Waandishi: SEI, Climate Analytics, E3G, IISD, UNEP
Jalada

Ripoti ya Pengo la Juhudi za Kukabiliana na Gesi Chafu — iliyozinduliwa mara ya kwanza mwaka wa 2019 — inafuatilia pengo liliopo kati  ya mipango ya serikali kuhusu uzalishaji wa mafuta ya kisukuku na viwango vya kimataifa vya uzalishaji vinavyolenga  kupunguza ongezeko la joto lisizidi nyuzijoto 1.5 au nyuzijoto 2.

Ni yepi mapya katika ripoti ya mwaka huu?

Ripoti ya Pengo la Juhudi za Kukabiliana na Gesi Chafu mwaka wa 2023: "Kupunguza au kuongeza? Wazalishaji wakuu wa mafuta ya visukuku wanapanga kuzalisha zaidi licha ya ahadi za kushughulikia mazingira" inaonyesha kuwa serikali zinapanga kuzalisha takriban asilimia 110 zaidi ya mafuta ya visukuku katika mwaka wa 2030 kuliko inavyotakiwa kudhibiti ongezeko la joto lisizidi nyuzijoto 1.5, na asilimia 69 zaidi ya inavyohitajika kudhibiti ongezeko la joto lisizidi nyuzijoto 2.

Ripoti hii inatoa taarifa mpya kwa mapana kuhusu nchi 20 ambazo ni wazalishaji wakuu wa nishati ya visukuku:  Australia, Brazil, Kanada, Uchina, Colombia, Ujerumani, India, Indonesia, Kazakhstan, Kuwait, Meksiko, Nigeria, Norway, Qatar, Urusi, Saudi Arabia, Afrika Kusini, Miliki za Falme za nchi za Kiarabu, Uingereza ikijumuisha Uingereza na Ireland Kaskazini, na Marekani.Maelezo haya yanaonyesha kuwa nyingi ya serikali hizi zinaendelea kutoa msaada muhimu wa kisera na wackifedha kwa uzalishaji wa mafuta ya visukuku.

“Hatuwezi kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi bila kushughulikia chanzo chake: kutegemea nishati ya visukuku. COP28 ni sharti ipitishe ujumbe unaoeleweka wazi kwamba hatuwezi kuendelea kutumia nishati ya visukuku — kwamba mwisho wake umetimia.  Tunahitaji ahadi za kuaminika ili kuimarisha matumizi ya nishati jadidifu, kukoma kutumia nishati ya visukuku, na kuimarisha ufanisi wa nishati, huku tukihakikisha mabadiliko ya haki na ya usawa," alisema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.

Ripoti ya Pengo la Juhudi za Kukabiliana na Gesi Chafu mwaka wa 2023

Ripoti ya Pengo la Juhudi za Kukabiliana na Gesi Chafu mwaka wa 2023: "Kupunguza au kuongeza? Wazalishaji wakuu wa mafuta ya visukuku wanapanga kuzalisha zaidi licha ya ahadi za kushughulikia mazingira" inatathmini mipango na makadirio ya serikali ya kuzalisha makaa ya mawe, mafuta, na gesi na viwango vya kimataifa kwa kuzingatia malengo ya Mkataba wa Paris wa halijoto.