Licha ya wajibu wake muhimu wa kupunguza mabadiliko ya tabianchi na kutoa huduma muhimu za mifumo ya ekolojia, mboji inakabiliwa na vitishio vikubwa na kusalia kuwa miongoni mwa mifumo ya ekolojia isiyoeleweka vyema na isiyofuatiliwa sana ulimwenguni.
Atlasi ya Maeneo Makuu ya Mboji Duniani Mwaka wa 2024 hutathmini hali ya sasa ya maeneo ya mboji kote duniani na kuangazia vitisho vinavyoyakabili kuanzia kwa ukuaji wa miji, ukuaji wa viwanda, mabadiliko ya matumizi ya ardhi, na mabadiliko ya tabianchi. Kwa kuandaa mfululizo wa ramani zinazochambua usambazaji wa kimataifa wa mboji kuhusiana na data ya kijiografia kuhusu vitishio hivi, Atlasi hii inatoa muhtasari wa kina wa maeneo yalio hatarini.
Kama kifaa muhimu cha Mpango wa Mboji Duniani, Atlasi hii hutumika kama zana muhimu kwa wafanya maamuzi, hutoa data, ushahidi, na maarifa wazi kuhusu hali ya kimataifa ya mboji. Kwa kuziba pengo kati ya sayansi na sera, inabainisha vitisho na fursa, na kuwezesha maamuzi sahihi yanayotoa kipaumbele kwa usimamizi wake endelevu. Zaidi ya hayo, Atlasi hii inaangazia uwezekano wa kimataifa wa uhifadhi na uboreshaji wa maeneo ya mboji, kwa kuzingatia maeneo ambayo yanaweza kuathiriwa hasa na upangaji na maendeleo katika siku zijazo.
Kwa kuzingatia Tathmini ya Mboji Duniani na Ramani ya Mboji Duniani ya 2.0 inayoandamana nayo, iliyotolewa katika mwaka wa 2022, Atlasi hii inaonyesha ramani zilizosasishwa na kufanyiwa marekebisho za maeneo makuu ya mboji. Inajumuisha mada mbalimbali, ikijumuisha bayoanuai na utajiri wa spishi, maeneo yanayolindwa, mboji za milima na kwa ardhi iliyoganda, mboji za maeneo kame na maeneo kame kwa kiasi fulani, mabomba ya maji na uharibifu wa ardhi, uzalishaji wa GHG, miundomsingi mikuu na ukuaji wa miji, kilimo, ukuaji wa viwanda (k.m., madini, mafuta na gesi), mafuriko, maporomoko ya ardhi, mioto, na kadhalika.
Atlasi ya Maeneo Makuu Ya Mikoko Duniani iliyozinduliwa tarehe 21 Novemba mwaka wa 2024, ni mwito wa kuchukua hatua - sio tu za kulinda mfumo wa ekolojia, lakini pia kutambua mwelekeo wa binadamu na kuelewa jinsi hatima ya mboji inavyohusishwa kimsingi na mustakabali wa sayari yetu na watu wake. Inaweka maeneo ya mboji mahali mwafaka: kitovuni mwa ajenda ya kimataifa ya mazingira. Wakati wa kuchukua hatua ni sasa, na Atlasi hii inaashiria hatua muhimu za kuwezesha kulinda mifumo hii ya ekolojia ili kuhakikisha inaendelea kusaidia vizazi vijavyo.