Ripoti ya Jukwaa la Kimataifa la Sera ya Sayansi Kuhusiana na Bayoanuai na Huduma za Mifumo ya Ekolojia (IPBES) inaangazia uhusiano uliopo kati ya uharibifu wa mazingira na ongezeko la magonjwa tandavu. Inakadiria gharama ya magonjwa tandavu na gharama ya kuzuia magonjwa tandavu katika siku zijazo na kupendekeza sera zinazozingatia sayansi kwa serikali na watoa uamuzi ili kuepuka magonjwa tandavu.