Kwa nini elimu na mazingira ni muhimu?

In Youth, education & environment

Maono yetu ni kuchochea kizazi kijacho cha viongozi vijana kuwa watu wanaojali mazingira na kupenda sayari mno. 

Kwa madhumuni haya, tunaamini kwamba elimu kuhusu mazingira na elimu kuhusu maendeleo endelevu ni uwekezaji muhimu, hasa ikiwa tunataka kutimiza Malengo ya Kimataifa.

Lakini zaidi ya hayo, maono yetu ni kufanya "idadi kubwa ya vijana", kuwa "vijana walio na maarifa" na kotoa fursa mpya za kazi zisizochafua mazingira, njia mpya za kufikia watu kupitia majukwaa ya michezo ya video, mbali na kufanya kazi na wabia wa Vyuo Vikuu ili kuunga mkono uongozi wao kote duniani.

Malengo ya Maendeleo Endelevu ni nguzo yetu kwa kazi hii, pamoja na kujitolea kusaidia watu kuishi maisha endelevu zaidi na kusaidia utoaji wa elimu ya mazingira kwa vijana. Ikiungwa mkono na serikali kote ulimwenguni, UNEP ina jukumu la wazi la kukuza ajenda hii na kuwawezesha vijana kuwa viongozi wa kesho.

In Youth, education & environment