New York, Septemba 22 , 2019 – Ili kuimarisha juhudi za kushughulikia mazingira na kudumisha uendelevu, benki maarufu zikishirikiana na Umoja wa mataifa zilizindua Kanuni za Uendeshaji Mzuri wa Shughuli za Benki, ambapo jumla ya benki 130 zilizo na mali ya jumla ya thamani ya dola za Marekani trilioni 47, au theluthi moja ya sekta ya benki duniani, zilitia sahihi.
Katika Kanuni hizo, zilizozinduliwa siku moja kabla ya Mkutano Mkuu wa Kushughulikia Mazingira wa Umoja wa Mataifa mjini New York, benki zimeahidi kujitolea kuendesha biashara zake kwa kuzingatia malengo ya Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na Malengo ya Maendeleo Endelevu, na kufanya juhudi za kasi ili kufikia malengo yote.
Kwa kutia sahihi kwa Kanuni hizi, benki zilisema kuwa zina imani kuwa "ni jamii zisizobagua tu zenye misingi yake katika kudumisha ubinadamu, kudumisha usawa na kutumia mali ghafi kwa njia endelevu" ndizo zinazowezesha wateja, wanunuzi na biashara zake kustawi.
Wakati ambapo viongozi kutoka pembe zote za duinia wanapokuja pamoja kushiriki yale wanayofanya ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu na kushughulikia mabadiliko ya tabianchi jumaa hili mjini New York, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, wakati wa tukio hilo la uzinduzi, lililohudhuriwa na Waanzilishi 130 waliotia sahihi zao na zaidi ya Afisa Wakuu Watendaji wake (CEOs) 45, alisema kuwa Kanuni za Uendeshaji Mzuri wa Shughuli za Benki za Umoja wa Mataifa, zinatoa mwongozo kwa sekta ya benki kushughulikia, kuendesha na kunufaika kutokana na maendeleo ya uchumi endelevu. Kanuni hizo zinahakikisha uwajibikaji unaoweza kupelekea uendeshaji mzuri na msukumo utakayowesha kuchukua hatua."
Kanuni hizo zinakuzwa kutokana na mfumo mkuu wa utelelezaji unaoweka wazi jinsi ya kuwajibika na kuitaka kila benki kuweka malengo, kuyasambaza na kuyafanyia kazi ili kuyatekeleza. Kwa kuweka utaratibu wa pamoja unaotoa mwongozo kwa benki ya jinsi ya kukuza biashara yake na kupunguza madhara kwa kukuza na kuleta mabadiliko yanayohitajika kwa mifumo ya uchumi na ya kijamii kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Kanuni hizi zinatoa fursa ya keleta mageuzi yatakayoweza kufanya shughuli za benki kwa njia endelevu.
“Sekta ya benki inayoweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazohusishwa na mabadiliko ya tabianchi na changamoto zinginezo zinazokabili mazingira inaweza kuleta mabadiliko yatakayopunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa na kukuza uchumi unaoweza kustahimili hali ya tabianchi," alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. "Iwapo mifumo ya kifedha itasitisha kuwa na tamaa ya fedha na kuacha kuwekeza katika sekta zinazosababisha uchafuzi na kukumbatia mifumo inayoleta suluhisho kwa changamoto za mazingira, kila mtu atakuwa mshindi hatimaye.”
Ijapokuwa idadi ya watu wanaoshughulikia mazingira inaongezeka, bado haijafikia kiwango kinachohitajika ili kufikia malengo ya Mkataba wa Paris wa nyusi joto 1.5. Wakati uo huo, bayoanuai inaendelea kuharibika katika kiwango kinachotia wasiwasi na mamilioni ya watu hupoteza maisha kila mwaka kutokana na uchafuzi wa hewa.
Kujitolea zaidi, ikijumuishwa pamoja na mabadiliko ya uwekezaji kutoka katika sekta ya kibinafsi, ni muhimu ili kukabiliana na changamoto hizi na kuhakisha kuwa hakuna yeyote anayebaguliwa wakati wa kushiriki rasilimali katika sayari yote.
Sekta ya benki na sekta za kibinafsi zinaweza kunafaika wakiwekeza wake kuhakikisha mageuzi haya
yatatimizwa. Inaaminiwa kuwa iwapo tutafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kuna uwezekano wa kupata faida ya dola za Marekani trilioni 12 kutoka kwa biashara na mapato kila mwaka na kubuni nafasi za kazi zaidi ya milioni 380 ifikiapo mwaka wa 2030.
"Ili kukumbatia uchumi unaozalisha hewa ya ukaa kwa kiasi kidogo na uchumi unaoweza kustahimili hali ya tabianchi na nia ya kutimiza malengo ya Mkataba wa Paris tunahitaji uwekezaji zaidi wa takribani dola za Marekani trilioni 60 kuanzia sasa hadi mwaka wa 2050," alisema Christiana Figueres, aliyeanzisha kampeni ya 'Mission 2020', anayepongezwa kwa kuandaa Mkataba wa Paris alipokuwa akihudumu kama Katibu Mkuu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (UN Framework Convention on Climate Change.) "Wakati sekta ya benki inapotoa zaidi ya asilimia 90 ya fedha katika nchi zinazoendelea na zaidi ya theluthi mbili kote ulimwenguni, Kanuni hizi ni hatua muhimu ili kufikia vigezo muhimu vya maendeleo endelevu katika sekta ya fedha.
MAKALA KWA WAHARIRI
Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa
UNEP ni msemaji mkubwa wa kimataifa kuhusu mazingira. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika kutunza mazingira kupitia kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.
Kuhusu Kanuni za Uendeshaji Mzuri wa Shughuli za Benki
Kanuni za Uendeshaji Mzuri wa Shughuli za Benki zilibuniwa na kikosi kutoka kwa benki 30 kupitia kwa mbinu bunifu ya ubia kati ya benki na Programu ya Ufadhili wa UNEP (UNEP FI). (UNEP FI) ni ushirikiano wa Umoja wa Mataifa na sekta za kibinafsi na ina wanachama kutoka kwa kwa zaidi ya taasisi za kifedha 240 kote duniani.
Ili kupata orodha kamili ya benki zote ambazo zilitia sahihi zao kama waanzilishi wa Kanuni za Uendeshaji Mzuri wa Shughuli za Benki na kupata nukuu kutoka kwa Afisa Wakuu Watendaji (CEOs) , tafadhali bonyezahapa.
Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea:
https://www.unepfi.org/banking/bankingprinciples/
Kwa maelezo zaidi na iwapo unahitaji mahojiano, tafadhali wasiliana na:
Nader Rahman, Meneja wa Mawasiliano (New York), nader.rahman@un.org, +1 (718) 517-1684
Simone Dettling, Mwakilishi wa Kikosi cha Benki, UNEP FI, Simone.dettling@un.org, +41 229178721
Keishamaza Rukikaire, Mkuu wa Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, rukikaire@un.org