Nairobi, Machi 30, 2021 — Uchafuzi wa plastiki huathiri jamii zilizotengwa na jamii zinazoishi katika maeneo ambayo plastiki huzalishwa kwa viwango vinavyotofautiana, hali isiyofanyia mazingira haki, kulingana na ripoti mpya ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na shirika lisilo la serikali la haki ya mazingira, Azul. Ripoti, YALIYOPUUZWA: Athari za Uchafuzi wa Bahari na Uchafuzi wa Plastiki kwa Haki ya Mazingira, inatoa wito wa kutambua jamii zilizoathiriwa na uchafuzi wa plastiki na kuzijumuisha wakati wa kufanya maamuzi.
Inaangazia visa vya kutofanyia mazingira haki – kuanzia kwa ukataji wa miti na kupoteza makao kwa watu wa kiasili ili kupata nafasi ya uchimbaji wa mafuta na uchafuzi wa maji ya kunywa kutokana na viti vioevu kutoka na uchimbaji wa mafuta Marekani na Sudan, hadi kwa matatizo ya kiafya kati ya jamii za Waafrika wengi wanaoishi karibu na maeneo ya kusafishia mafuta katika Ghuba ya Meksiko nchini Marekani, na hatari za kazini kwa takribani waokota taka milioni mbili nchini India, na kadhalika.
Taka ya plastiki haihatarishi kipato cha wale wanaotegemea tu malighafi kutoka baharini kama ajira, pia inaweza kupelekea changamoto za kiafya kwa watu wanaotumia chakula kutoka baharini kilicho na chembechembe za plastiki zilizo hatari. Changamoto za uchafu wa plastiki – ambazo zimezidishwa na janga la COVID-19 – ni sehemu kuu ya changamoto za uchafuzi duniani, ambazo mbali na uharibifu wa bayoanuai na mabadiliko ya tabianchi, huashiria masuala matatu ya dharura duniani yanayopaswa kushughulikiwa kwa kubadili mno jinsi binadamu wanavyotumia malighali duniani.
"Haki ya mazingira inamaanisha kuelemisha wanaosababisha uchafuzi wa plastiki mno kuhusu hatari yake, kuwajumuisha wakati wa kufanya maamuzi kuhusu uzalishaji, matumizi, utupaji wa plastiki ns kuhskikisha kuwa wanaweza kupati haki kisheria," alisema Katibu mtendaji wa UNEP, Inger Andersen.
Waandishi wa ripoti hiyo wanapendekeza kuwa serikali ziimarishe ufuatiliaji wa plastiki, wafanye tafiti kuhusu athari yake kwa afya, na kuwekeza kwenye ushuhulikiaji wake. Serikali zinapaswa pia kupitisha na kuimarisha utekelezaji wa marufuku ya plastiki inayotumika tu mara moja na kuhimiza kupunguzwa, kuundia bidhaa tena na kutumia tena. Kwa kuongezea, zinapaswa kuhamasisha na kushawishi jamii zilizoathiriwa kuchukua hatua kwa kuhakikisha kuwa wanaweza kupata haki ya kisheria kikamilifu kwa kufuata kanuni za haki kwa mazingira, kukubali kushiriki kwa hiari (FPIC), na haki ya kupokea taarifa.
Mwandishi Mwenza, Mwanzilishi na Katibu Mtendaji wa Azul, Marce Gutiérrez-Graudiņš, alisema: “Uchafuzi wa plastiki ni suala la haki katika jamii. Juhudi za sasa za kushughulikia na kupunguza uchafuzi wa plastiki hazitoshi kukabiliana na tatizo hili kabisa. Athari zinazotaufautiana kwa jamii zilizoathiriwa na plastiki, katika ngazi zote kuanzia kwa uzalishaji hadi kwa taka, zinapaswa kufanya haki kwa mazingira kuwa suala la kawaida katika uhifadhi wa maeneo ya baharini.”
Ripoti hiyo inafuata Azimio 2/11 la Baraza la Mazingira la UNEP la kufanyia utafiti zaidi athari za plastiki kwa mazingira, kwa afya na kwa jamii. Inaonyesha jinsi ambavyo plastiki inadidimisha uwezo wa kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hasa SDG1 kuhusiana na umaskini, SDG2 kuhusiana na baa la njaa, SDG14 kuhusiana na utunzaji wa mifumo ya ekolojia ya baharini, na SDG16 kuhusiana na kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wote, na kujenga taasisi mwafaka, zinazowajibika na zisizobagua katika ngazi zote.
"Athari ya plastiki kwa jamii zilizo hatarini zaidi kuathirika ni zaidi ya kutoshughulikia plastiki ipasavyo na wakati mwingine ukosefu wa mifumo ya kushughulikia taka," amesema Juliano Calil, mwandishi mkuu wa ripoti na Mtafiki Mkuu anayefadhiliwa na Kituo cha Blue Economy. "Inaanza na masuala yanayohusiana na uchimbaji wa mafuta, hadi kwa mazingira hatari na uzalishaji wa gesi ya ukaa, na hata kuathiri sera za usambasaji wa maji."
Makala kwa Wahariri
Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa
UNEP ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.
Kuhusu Azul
Azul ni shirika lisilo la serikali la haki ya mazingira linalofanya kazi na jamii nyanjani kutunza maeneo ya pwani na bahari. Shirika lililoanzishwa katika mwaka wa 2011, Azul limeendeleza na kutekeleza kampeni ambazo zilipata ushindi kuhusiana na sera za kuhifadhi bahari.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Keisha Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa