Umekuwa msimu mwingine wa hali mbaya zaidi ya hewa, na kila kitu kuanzia na kiwango cha juu cha joto hadi kwa mafuriko mabaya zaidi yanayokabili nchi kote ulimwenguni. Lakini mojawapo ya mielekeo inayotisha zaidi ni kile wanasayansi wamekiita wimbi la joto baharini duniani ambalo halijawahi kutokea.
Mwezi wa Juni ulishuhudia wastani ya juu zaidi ya kiwango cha joto baharini, huku viwango duniani katika maeeneo vikiwekwa kuanzia kwa Ireland hadi Antaktika. Mjini Florida, maji yalifikia nyuzijoto 38. Bahari ya Atlantiki ya Kaskazini ilirekodi kiwango cha zaidi the joto katika mwezi wa Julai. Na Bahari ya Mediterania iligonga nyuzijoto 28.7, kiwango cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa.
Kwa hivyo, kwa nini kiwango cha joto baharini kinaongezeka zaidi? Wataalamu wanasema ni kutokana na mchanganyiko wa mambo, kuanzia kwa janga la mabadiliko ya tabianchi hadi kwa upepo wa kutisha katika Jangwa la Sahara. Pia wanasema kuwa viwango vya joto vya juu vina athari kubwa kwa viumbe wa baharini na kwa binadamu.
"Athari za mawimbi ya joto baharini ni hutofautiana na zinadhuru sana," alisema Leticia Carvalho, Mkuu wa Mifumo ya Maji Safi na Mazingira ya Baharini katika Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). "Tunajua kupanda kwa joto kali kunaweza kusababisha vifo vingi vya viumbe vya baharini, kuongeza asidi baharini na kuharibu mikondo inayoathiri mifumo yetu ya hali ya hewa, ambayo inaweza kusababisha hasara ya mamilioni ya dola kwa uchumi na kusababisha hatari kubwa kwa utoshelezaji wa chakula duniani."
Kiwango cha joto baharini kiliongezeka kati ya mwaka wa 1982 na 2016 na kinaendelea kuongezeka na kushuhudiwa kwa kipindi kirefu kwa mjibu wa utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Jopo la Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi.
Mawimbi ya joto la hivi karibuni linasababishwa na mabadiliko ya tabianchi, alisema Carvalho. Wakati binadamu wanavyochoma nishati ya mafuta, kiasi kikubwa cha gesi ya ukaa inayozidisha joto kwenye sayari zinajaa angani. Sehemu kubwa ya joto hilo hufyozwa na bahari.
Hali hii haipelekei tu viwango vya juu vya joto baharini, bali pia hufanya bahari kuwa na ufanisi mdogo katika kufyonza kaboni dioksidi, na kuacha gesi zaidi ya ukaa kuzunguka angani.
Janga la janga la mabadiliko ya tabianchi huchangiwa na muundo asilia wa tabianchi wa El Niño unaoendelea kwa sasa, unaoongeza joto baharini katika Bahari ya Pasifiki.
Pia, kuna sababu zingine za wimbi la joto bahari. Upepo dhaifu kuliko wastani umepunguza kiwango cha vumbi la Sahara angani, ambayo kwa kawaida hupunguza joto baharini kwa kuzuia baadhi ya nguvu za jua.
Viwango zaidi vya joto baharini vinaweza kuwa na athari mbaya kwa viumbe vya baharini, na kumekuwa na vifo vingi vya wanyama na mimea baharini kutokana na mawimbi ya joto ya baharini.
Mfano mmoja ni vifo vya umati wa Kaa wa maeneo ya Theluji wa Alaska katika Bahari ya Bering, ambapo idadi ya watu ilipungua kutoka takriban bilioni 11 hadi chini ya bilioni 2 katika kipindi cha miaka minne. Kutokana na hali hii, jimbo la Alaska nchini Marekani lilifunga msimu wa kaa wa maeneo ya theluji kwa mara ya kwanza katika mwezi wa Oktoba mwaka wa 2022.
Mawimbi ya joto yanaweza pia kudhuru mwani unapochanua, uchuchukaji wa matumbawe, kupoteza makao kwa viumbe vya baharini - wanapotafuta maji baridi zaidi - na usumbufu kwa mifumo yao ya chakula. UNEP inakadiria kuwa asilimia kati ya 25 na 50 ya miamba ya matumbawe duniani imeharibiwa, na kwamba miamba yote ya matumbawe itakuwa imengamia kufikia mwaka wa 2100 ikiwa uuzalishaji wa gesi ya ukaa hautakatwa kwa kiasi kikubwa.
Kuongezeka kwa joto baharini kunaweza kudhuru nchi kavu pia, na kusababisha hali mbaya ya hewa, kama vile dhoruba na vimbunga.
Kadiri kiwango cha joto majini kinavyoongezeka - wastani wa joto baharini imeongezeka kwa nyuzijoto 1.5 katika karne iliyopita - uwezo wa mifumo ya ekolojia ya maeneo ya bahari kunyonya ongezeko la joto katika eneo umepunguka, na hivyo kuongeza uwezekano wa mawimbi ya joto zaidi baharini.
Bahari ni mfuonzaji muhimu wa gesi ya ukaa," Carvalho anasema. "Hufyonza asilimia 90 ya joto la ziada linalotokana na uzalishaji wa kabonikisidi na kutupa asilimia 50 ya oksijeni tunayohitaji. Ni mapafu ya sayari, na hudhibiti hali yetu ya hewa. Walakini, iko hatarini zaidi na tunahitaji kuweka kipaumbele mara moja kwa juhudi za utunzaji na uboreshaji wake."
Hali mbaya zaidi inaweza kuwa haijaisha, huku Usimamizi wa Kitaifa wa Bahari na Anga ya Amerika ukionya kwamba nusu ya bahari ulimwenguni inaweza kushuhudia mawimbi ya joto kufikia Septemba. Na bila dalili ya kupungua kwa uzalishaji wa hewa chafu duniani, matukio haya mabaya ambayo mara nyingi yanaweza kutokea zaidi katika miaka ijayo.
Sehemu moja ya dunia inayozidi kuwa hatarini zaidi kukabiliwa na mawimbi ya joto baharini ni Antaktika, ambayo ina wajibu muhimu katika kudhibiti mfumo wa hali ya hewa Duniani.
Tangu mwaka wa 1992, Antaktika imekuwa ikipoteza karibu tani bilioni 100 za barafu kwa mwaka, na mwaka huu ilishuhudia kiwango cha chini kabisa cha barafu, ilipungua kwa takribani kilomita mraba milioni 2.6 ikilinganishwa na wastani ya miaka ya 1981 hadi 2010.
Kupungua kwa barafu baharini haimaanishi tu kuongezeka kwa kiwango cha bahari katika siku zijazo, inamaanisha kuwa kuna barafu kidogo kuakisi nishati ya jua, hali inayopelekea ongezeko la joto baharini na mawimbi ya joto baharini kutokea mara kwa mara, hali mbaya inayojirudia ambayo inayoweza kuwa na athari kote ulimwenguni.
"Msimu huu wa kiangazi kwa kweli unahitaji kutuamsha kwa ukweli kwamba athari za mabadiliko ya tabianchi zinashuhudiwa katika mifumo yote ya ekolojia katika kila pembe ya dunia," anasema Carvalho. "Kuna haja ya kupunguza uzalishaji wa hewa chafu, lakini pia uwekezaji zaidi katika masuluhisho ya kiasili pamoja na utafiti zaidi katika ufuatiliaji wa mawimbi ya joto baharini."
Sekta Sita za Kusuluhisha janga la mabadiliko ya tabianchi
UNEP iko mstari mbele kuunga mkono lengo la Mkataba wa Paris la kudhibiti kiwango cha joto duniani kisizidi nyuzijoto 2, na kulenga nyuzijoto 1.5, ikilinganishwa na viwango vya kabla ya viwanda. Ili kufikia lengo hili, UNEP imeunda mwongozo wa Masuluhisho katika Sekta Sita, ya kupunguza uzalishaji wa hewa chafu katika sekta mbalimbalikwa kuzingatia ahadi katika Mkataba wa Paris ili kuwezesha kuwa na mazingira thabiti. Sekta sita zilizoainishwa ni: nishati; viwanda; kilimo na chakula; misitu na matumizi ya ardhi; uchukuzi; na ujenzi na miji.