Photo by Kéré Architecture/Enrico Cano
28 May 2024 Tukio Miji

Mbinu za kitamaduni za ujenzi hutoa masuluhisho endelevu huku miji barani Afrika inapokua

Photo by Kéré Architecture/Enrico Cano

Shule inayopatikana kwa viunga vya vumbi nyingi vya mji wa Koudougou nchini Burkina Faso, Shule ya Sekondari ya Lycée Schurge inaonyesha kile kinachoweza kutokea unapochanganya mbinu za kitamaduni na nyenzo mpya.

Shule hii ina mizunguko tisa zilizopangwa karibu na ua mkuu, ili kulinda maeneo makuu dhidi ya upepo na vumbi. Kila mzunguko umejengwa kutoka kwa ngegu inayopatikana katika eneo hili, ambayo hukatwa kuwa matofali na kuachwa kwa jua ili kuwa magumu. Matofali haya huhifadhi joto wakati wa mchana na kuliachilia usiku. 

Majengo pia yameundwa kwa maganda kutoka kwa miti mbao ambayo yamefunika na kuzunguka madarasa kama kitambaa unachoweza kuona kupitia na kutengeneza maeneo mbalimbali yalio na kivuli ili kuwalinda wanafunzi dhidi ya joto la mchana la kudumaza.

Jengo hili, lililoundwa na kampuni ya usanifu yenye makao yake makuu mjini Berlin ya Mburkinabè ya Kéré Architecture, ni mfano wa jinsi nchi barani humu zinavyotumia mbinu za jadi za ujenzi ili kupunguza kiwango cha hewa ya ukaa cha majengo yao. 

Utafiti unaonyesha kuwa mbinu hizi zinaweza kusaidia kuzuia hitaji la viyoyoziusafirishaji wa masafa marefu wa vifaa vya ujenzi na utengenezaji wa saruji, yote haya yanayochangia uzalishaji wa gesi ya ukaa (GHG) unaochangia janga la mabadiliko ya tabianchi.

The Naaba Belem Goumma Secondary School being built
Shule ya Sekondari inayojengwa ya Naaba Belem Goumma. Picha:  Usanifu wa Kéré |

Huku asilimia 70 ya majengo barani Afrika ambayo yatakuwepo kufiki mwaka 2040 bado hayajajengwa, wataalam wanasema mbinu hizi za kuokoa nishati ni muhimu. 

"Mbinu za ujenzi na majengo endelevu za kijadi ni nguzo ya urithi wa kitamaduni barani Afrika," anasema Jonathan Duwyn, kutoka kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). "Miundo, ujenzi, mazoea, na nyenzo endelevu zilizofanyiwa mabadiliko pamoja na vitu mbadala na uvumbuzi vinawakilisha fursa kubwa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kustahimili hali barani Afrika ambapo ujenzi unaongezeka kwa kasi."

UNEP ilishiriki katika mradi wa Burkina Faso, kwa ushirikiano na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Huduma za Miradi na UN Habitat. 

Afrika huchangia takriban asilimia 6 ya mahitaji ya nishati duniani, huku zaidi ya nusu ya kiwango hili ikitoka kwa majengo yake. Ikizingatiwa kuwa idadi ya watu barani Afrika inatarajiwa kufikia watu bilioni 2.4 kufikia mwaka wa 2050, huku asilimia 80 ya ukuaji huu ikitokea mijini, uendelevu unahitaji kuwa kanuni ya msingi ya majengo yote yajayo, wanasema wataalam. 

Masuluhisho haya yameangaziwa katika Ripoti ya Hali ya Kimataifa ya Majengo na Ujenzi ya mwaka wa 2022 ya UNEP, iliyozinduliwa katika Kongamano la Umoja wa Mataifa la Tabianchi (COP27) nchini Misri. Ripoti hiyo iliangazia jinsi Afrika inavyoweza kushughulikia ukuaji huu wa miji na kuongeza ustahimilivu wa majengo yake ya makazi huku ikiepuka kuongeza kwa uzalishaji wa GHG.

Msukumo wa ujenzi unaostahimili hali ya hewa unaweza kupatikana katika historia yote ya Afrika. Safiri barani Afrika leo, na vidokezo vyake vya kuwepo tangu zamani vinaweza kupatikana kila mahali, kutoka kwa vibanda vya mizinga ya nyuki vya Eswatini hadi vijiji vya miamba ya Drogon nchini Mali hadi kwa misikiti ya matofali ya matope ya Afrika Magharibi.

"Afrika ina utajiri mkubwa wa vyanzo vya nishati jadidifu, ya jua na upepo, huku karibu nusu ya uwezo wa nishati jadidifu duniani ukiwa Afrika," Duwyn anasema. 

Hili ni muhimu hasa kutokana na makadirio ya mahitaji ya viyoyozi huku watu wengi zaidi wanapopata umeme na kutokana na ongezeko la joto. "Tunatarajia kupunguza kuwa changamoto kubwa kuhusiana na suala la mahitaji ya nishati ya maeneo ya makazi barani Afrika katika siku zijazo, anasema Duwyn. "Ndio sababu ni muhimu sana kuhakikisha majengo mapya yanatumia mifumo ya kiasili ya kupunguza joto inapowezekana."

Lycee Schorge secondary school
Shule ya Sekondari ya Schurge nchini Burkina Faso. Picha: Usanifu wa Kéré /Iwan Baan

Mradi mwingine wa Usanifu wa Kéré unaotumia muundo endelevu na mazoea endelevu ya ujenzi ni shule ya msingi ya Gando. Imejengwa kwa matofali ya mchanganyiko wa udongo/saruji kama dari ya matofali - badala ya paa la kawaida la mabati -ili kuruhusu uingizaji hewa wa kiwango cha juu kwa njia za kiasili. 

"Miradi hii inaonyesha kwamba mbinu endelevu za ujenzi zinawezekana mbinu za kibunifu zinapotumika," anasema Duwyn. "Na hali ya hewa barani Afrika inapozidi kuwa na joto zaidi, ni muhimu kukumbatia miundo endelevu ya majengo ambayo haihitaji mifumo ya kupunguza joto ya gharama za juu na iliyo na uharibifu." 

Kama Ripoti ya Hali ya Ujenzi Ulimwenguni inavyoangazia, Afrika ina utajiri wa nyenzo asilia, endelevu kama vile matofali ya udongo, ngegu, udongo wa kilima cha mchwa, mbao, mawe, mianzi, mchanga na mimea iliyokauka. Mbinu za jadi za ujenzi ni pamoja na kushindilia udongo, matofali yaliyokaushwa kwa jua, mabloku yalioshindiliwa, kibanda cha fito kilichokandikwa, bunzi, ujenzi wa kutumia mbao, ujenzi wa kutumia mchanga na paa za nyasi. 

Kuhakikisha nyenzo endelevu zinatumika ni muhimu hasa, ikizingatiwa kwamba kulingana na UNHabitat, zaidi ya nusu ya idadi ya, wakazi Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaishi katika makazi yasiyo rasmi yalio na idadi kubwa wa watu, ambao huathirika zaidi na athari za mabadiliko ya tabianchi.

"Makazi bora endelevu ni njia muhimu ya kuhakikisha kuwa watu watu walio hatarini zaidi wanastahimili zaidi athari za janga la mabadiliko ya tabianchi," Duwyn anasema. 

Maakala haya yalichapishwa kwa mara ya kwanza tarehe 22 Novemba mwaka wa 2022 na yamesasishwa.