Mifumo mizuri ya ekolojia inaweza kupunguza madhara yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi. Kwa mfano mikoko inayopatikana katika maeneo ya Pwani huzuia mafuriko, maziwa yaliyohifadhiwa vizuri huhifadhi maji wakati wa kiangazi, na misitu iliyonawiri hupunguza uwezekano wa kutokea kwa mioto mibaya mno porini. Kukabiliana na hali kwa kuzingatia mifumo ya ekolojia (EbA) ni mbinu inayotumia hizi huduma za mifumo ya ekolojia kama sehemu ya mikakati mikuu ya kukabiliana na hali. Mara nyingi, kwa manufaa kwa wote, (EbA) husaidia jamii zilizo hatarini zaidi kuathiriwa na hali mbaya ya hewa na kwa wakati uo huo kupata manufaa muhimu kwa maisha ya binadamu, kama vile maji na chakula.