17 Sep 2020 Video Kutumia mazingira kushughulikia tabianchi

Shindano la 'Run Wild Challenge': Wakimbiaji milioni moja kuwakilisha spishi milioni moja zilizo hatarini kuangamia

Kampeni ya 'Run Wild' inaendeshwa kwa ushirikiano wa UNEP na adidas Runtastic wakiungwa mkono na Shirika la Internet of Elephants na wabia wa shughuli za kuhifadhi mazingira, ili kuhamasisha kuhusu kuharibika kwa bayoanuai na umuhimu wa kutunza wanyamapori wetu - lengo likiwa kuwafanya wakimbiaji milioni moja kushiriki ili kuwakilisha spishi milioni moja zilizo hatarini kuangamia.

https://www.youtube.com/watch?v=nwKQOy59W8U

Kwa kushiriki katika kampeni hii itakayoendeshwa kwa siku kumi, washiriki mbali na kupima uwezo wao wa kukimbia kwa kushindana na mnyama halisi - kakakuona, buka au ndovu - wanaweza pia kujielimisha kuhusu hawa wanyama wa ajabu na hatari wanayokumbana nayo kote duniani. Kampeni hii inafanywa kwa ushirikiano na wabia wa shughuli za kuhifadhi mazingira - Mashirika ya Pangolin Project, Space for Giants na Kituo cha Bhutan Tiger Center - yanayotoa data halisi ya GPS-inayofuatilia wanyama wanaoshiriki katika shindano la mbio. UNEP kupitia kwa programu yake ya Vanishing Treasures inashirikiana na Kituo cha Bhutan Tiger Center kinachosaidia kuhifadhi buka.