Tunahitaji mazingira iwapo tungependa kujenga na kuwa na dunia iliyostawi zaidi
Jamii zetu zina uhusiano wa kipekee na bayoanuai na huitegemea. Bayoanuai ni muhimu kwa binadamu, ikiwa ni pamoja na kuwapa chakula, maji safi, dawa, na kuwakinga dhidi ya majanga mabaya.
Kuharibika kwa bayoanuai na kudidimia kwa manufaa yake kwa binadamu, hupunguza uwezekano wa kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na kuathiri kipato cha watu. Kuna idhibati tosha ya kuonyesha uhusiano uliopo.
Nchi zinapoweka mikakati ya kujiimarisha baada ya janga la COVID-19, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bayoanuai, ulioandaliwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo tarehe 30, Septemba mwaka wa 2020, unatoa wito wa kufanya kazi kwa lengo moja, kuwezesha watu wote kuishi vizuri na mazingira. #TutunzeMazingira