08 November 2024 Ripoti

Jicho kwa Methani mwaka wa 2024

Waandishi: UNEP
cover

Uzalishaji wa methani unaosababishwa na binadamu unawajibikia takriban theluthi moja ya ongezeko la joto duiani kwa sasa. Kupunguza uzalishaji huu ndiyo njia ya haraka zaidi, ya gharama nafuu zaidi ya kupunguza ongezeko la joto duniani katika siku zijazo—na ni muhimu ili kuepusha madhara makubwa ya tabianchi. 

Toleo la nne la chapisho la UNEP la Uchunguzi wa Kimataifa wa Uzalishaji wa Methani (IMEO), Jicho kwa Methani, Haionekani lakini haimainishi haiko, inatathmini hatua zilizopigwa kukusanya data kubwa ya methani ambayo inaweza kuharakisha upunguzaji wa methani katika ngazi ya kimataifa. 

IMEO ya UNEP hutoa data na muktadha kwa watu binafsi wanaoweza kuchukua hatua za kupunguza uzalishaji wa hewa chafu. Ili kufanya hivyo, IMEO hukusanya na kuchapisha data kupitia kutoa ripoti kuhusu sekta kupitia Ushirikiano wa Mafuta na Gesi ya Methani 2.0 (OGMP 2.0), kutoka kwa setilaiti kupitia Mfumo wa Kuangazia na Kushughulikia Methani (MARS), kutoka kwa msururu wake wa tafiti za kisayansi za kimataifa kuhusu methani, na kutoka kwa orodha za kitaifa za uzalishaji wa hewa chafu.