Mwongozo wa Mawasiliano Kuhusu Mtindo Endelevu, uliochapishwa kwa ushirikiano wa UNEP na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi, unatoa dira, kanuni na mwongozo kuhusu jinsi ya kuoanisha mawasiliano yanayowalenga wateja katika sekta ya mitindo kote ulimwenguni na malengo endelevu.
Inaonyesha jinsi wanaowasiliana kupitia kwa mitindo - wauzaji, wasimamizi wa chapa, watengenezaji wa michoro, vyombo vya habari, washawishi na kadhalika - wanavyoweza kusaidia kuwezesha kufikia Mkataba wa Paris na Malengo ya Maendeleo Endelevu kupitia 1) kukabiliana habari potofu, 2) kupunguza ujumbe unaopelekea matumiz kupita kiasi, 3) kuelekeza hamu maishani kwa mitindo endelevu zaidi, na 4) kuwawezesha watumiaji kutoa wito wa uchukuaji wahatua kubwa zaidi kutoka kwa wafanyabiashara na watungasera.
Inatambua sekta ya mitindo kama mojawapo ya sekta muhimu duniani, ila husumbuka kukabiliana na athari zake kwa upana, na ruwaza isiyo endelevu ya matumizi na uzalishaji huchangia moja kwa moja na kwa kiasi kikubwa kwa changamoto za aina tatu duniani, pamoja na suala lililoingiliana la ukosefu wa haki katika jamii.
Ingawa kushughulikia athari za uzalishaji ni muhimu, kufanya hivyo pekee hakutoshi kuleta mabadiliko ya kutosha katika sekta hii kwa wakati unaohitajika. Kubadilisha ruwaza ya matumizi ni sharti kupewe kipaumbele, kumaanisha kukabiliana na mfumo mkuu wa kiuchumi unaofuata utaratibu mmoja na masimulizi yanayoambatana na upya, upesi na utupaji. Mwongozo huu unawaalika wote wanaowasiliana kupitia kwa mitindo kujadiliana, ikisisitiza kwa mara ya kwanza katika sekta hii umuhimu wa watambaji kama wawezeshaji na wachochezi wa mabadiliko ya kimfumo.
Rasilimali muhimu:
- Toleo ku kuwasiliana - mwongozo
- Shughuli za UNEP za Mawasiliano Kuhusu Mtindo
- Uendelevu na Matumizi ya Tena na Tena katika Mfumo wa Usambasaji wa Mavazi - Mwongozo wa Kimataifa
- Uendelevu na matumizi ya tena na tena katika sekta ya mavazi