Mambo mapya katika ripoti ya mwaka huu
Ripoti hii inaonyesha kuwa kuna hatua ambazo zimepigwa tangu Mkataba wa Paris ulipotiwa sahihi katika mwaka wa 2015. Uzalishaji wa gesi ya ukaa kufikia mwaka wa 2030 kwa kuzingatia sera zilizopo ulikadiriwa kuongezeka kwa asilimia 16 wakati wa kupitishwa kwa mkataba huu. Leo, makadirio ya ongezeko ni asilimia 3. Hata hivyo, makadirio ya uzalishaji wa gesi ya ukaa kufikia mwaka wa 2030 bado ni sharti yapungue kwa asilimia 28 ili kufikia malengo ya Mkataba wa Paris ya nyuzijoto 2 na kwa asilimia 42 ili kufikia nyuzijoto 1.5.
Mambo yakisalia jinsi yalivyo, utekeleza kikamilifu wa Ahadi Zinazowekwa na Taifa (NDCs) chini ya Mkataba wa Paris utawezesha ulimwengu kudhibiti ongezeko la joto hadi nyuzijoto 2.9 zaidi kuliko viwango vya kabla ya viwanda. Utelelezaji kikamilifu wa NDC zilizo na masharti unaweza kupunguza hadi nyuzijoto 2.5.
Ripoti hii inatoa wito kwa mataifa yote kuharakisha hatua za mabadiliko ya kupunguza hewa ya ukaa wakati wa maendeleo kwa uchumi wote. Nchi zilizo na uwezo mkubwa na huchangia zaidi kwa uzalishaji wa hewa chafu zitahitaji kuchukua hatua kabambe na kusaidia mataifa yanayoendelea yanapofanya juhudi za kupunguza hewa ya ukaa wakati wa kukuza uchumi.
Ripoti hii inaangazia jinsi utekelezaji madhubuti wa unavyoweza kuimarisha awamu inayofuata ya NDC ambazo nchi zinapaswa kuwasilisha katika mwaka wa 2025, ili kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa kufikia mwaka wa 2035 kurandana na viwango vya chini ya nyuzijoto 2 na nyuzijoto 1.5. Inaangazia pia uwezo na madhara ya mbinu za Uondoji wa Kaboni Dioksidi kama vile masuluhisho yanayotokana na mbinu za kiasili kunasa na kuhifadhi hewa ya ukaa moja kwa moja.