Mambo mapya katika ripoti hii
Ripoti hii inaangalia kiwango cha ahadi ambacho nchi zinapaswa kutoa ili kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa na kufikia malengo, katika awamu ijayo ya Michango Inayoamuliwa na Taifa (NDCs) inayotarajiwa kuwasilishwa mapema ya mwaka wa 2025 kabla ya COP30. Upunguaji kwa asilimia 42 unahitajika kufikia mwaka wa 2030, na asilimia 57 kufikia kufikia mwaka wa 2025 ili kuweza kufikia nyuzijoto 1.5.
Kushindwa kuongeza ahadi katika NDC hizi mpya na kuanza kuzitekeleza haraka kutafanya ulimwengu kuweza kushuhudia ongezeko la joto kati ya nyuzijoto 2.6 na 3.1 katika kipindi cha karne hii. Hali hii inaweza kusababishaathari mbaya zaidi kwa watu, sayari na uchumi.
Bado inawezekana kiufundi kufikia nyuzijoto 1.5, huku nishati ya jua, upepo na misitu ikishikilia ahadi ya kweli ya kupunguzwa kwa uzalishaji na utoaji wa hewa chafu haraka. Ili kutimiza uwezo huu, NDC thabiti za kutosha zitahitaji kuungwa mkono haraka na mbinu nzima inayozingatiwa na serikali, hatua zinazoongeza manufaa ya kijamii na kiuchumi na kimazingira kwa pamoja, ushirikiano ulioimarishwa wa kimataifa unaojumuisha mageuzi ya mfumo wa ufadhili duniani, hatua thabiti za sekta binafsi na angalau uongezekaji mara sita wa ufadhili wa kukabiliana na hali. Mataifa ya G20, haswa wanachama wanaozalisha hewa chafu zaidi, yanahitaji kufanya kazi nzito.