Report

Kutembea na Kuendesha Baiskeli Barani Afrika - Ushahidi na Mazoezi Mazuri ya Kuigwa

27 July 2022
Jalada la ripoti

Zaidi ya watu bilioni moja hutembea au kuendesha baiskeli barani Afrika kila siku ili kufika kazini, nyumba kwao, shuleni na kufikia huduma nyingine muhimu. Ingawa kumekuwa na hatua madhubuti na za kutia moyo kuimarisha hali kwa watu wanaotembea na wanaendesha baiskeli barani kote, nchi nyingi bado hazina sera, miundomsingi mwafaka na bajeti za kuwalinda watumiaji wa barabara walio hatarini. Hatari haiko tu barabarani, ila angani pia. Utoaji wa hewa chafu kutoka kwa magari, unaoongezeka, huchangia kwa janga la mabadiliko ya tabianchi na huwajibikaa kiwango kikubwa cha uchafuzi wa hewa nje ya majumba.

Barani Afrika, kwa wastani, watu hutumia hadi dakika 56 kutembea au kuendesha baiskeli kama njia ya usafiri kila siku, na kupita wastani wa kimataifa wa Dakika 43.9. Dakika hizi 56 za za kufanyisha mwili mazoezi za kila siku kama mbinu ya usafiri husababisha kelele na uchafuzi wa hewa kidogo zaidi, hauhitaji matumizi ya fueli ya visukuku na una manufaa makubwa ya kiafya.

KUHUSU RIPOTI

Ripoti hii ni jaribio la kwanza la kukusanya, kuchanganua na kuwasilisha data ili kuonyesha hali halisi ya kila siku kwa watu bilioni moja barani Afrika wanaotembea na kuendesha baiskeli kila siku.  Inaonyesha hali katika nchi zote 54 barani Afrika kwa kutumia vyanzo vya data vilivyopo vilivyofafanuliwa kupitia kutembea na kuendesha baiskeli na kuangazia mbinu bora zinazovutia. Inaangazia umuhimu wa kutoa kipaumbele kwa maisha ya watu wanaotembea na kuendesha baiskeli katika nchi barani Afrika kuwa salama, ya kudumisha afya na bora zaidi ikiwa tunataka kuhakikisha kuna miji bora iliyo na usawa zaidi.

Ripoti inatoa mapendekezo kwa serikali na washikadau wengine na kutoa wito wa kudumisha, kuwezesha na kulinda wale ambao tayari wanasafiri kwa njia endelevu iwezekanavyo. Imeandaliwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Shririka la Makazi la Umoja wa Mataifa (UNHabitat) na Wakfu wa Walk21, na inatoa ushahidi, maarifa na hatua muhimu zinazohitajika ili kuhakikisha maamuzi ya usafiri yanayofanywa leo yatapelekea mitandao salama, endelevu na thabiti atika siku za usoni.