Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Muungano wa Mazingira na Hewa Safi (CCAC) na Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA) wamechapisha tathmini ya manufaa kwa mazingira na kwa afya: "Umuhimu Kupunguza Methani kutoka kwa Nishati ya Visukuku".
Methani husababisha uchafuzi wa mazingira unaochangia takribani asilimia 30 ya ongezeko la joto duniani tangu nyakati za Mapinduzi ya Viwanda. Shughuli za nishati ya visukuku ni mchangiaji wa pili kwa ukubwa wa uzalishaji wa methani ya anthropojeniki, na wingi wa uchafuzi huu unaweza kupunguzwa kwa kutumia teknolojia iliyopo, mara nyingi kwa gharama za chini.
Ijapokuwa Kutozalisha Hewa Chafu Kabisa kufikia mwaka wa 2050 ilionyesha kuwa ongezeko kubwa la nishati isiochafua mazingira lilipunguza matumizi ya nishati ya visukuku, na hivyo kusababisha kupungua kwa uzalishaji wa methani; ripoti hii inapata kwamba hii haitoshi kupunguza utoaji wa methani kwa kasi na kwa kiwango kinachohitajika ili kuepuka athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi.
Zaidi ya hayo, ripoti hii inaangazia hatua zinazolengwa zinazohitajika ili kukabiliana na uzalishaji wa methani kutokana na uzalishaji na matumizi ya nishati ya visukuku, ili kupunguza hatari ya kutoweza kubadilisha athari mbaya kwa mazingira na kupelekea manufaa kwa afya ya umma.