07 February 2023 Ripoti

Kujiandaa kushughulikia vimelea sugu: Kuimarisha juhudi za kushughulikia mazingira kupitia mkakati wa ‘Afya Moja’

Waandishi: UNEP
picha

Vimelea sugu au AMR huchukuliwa kuwa mojawapo ya changamoto kuu kwa afya ya umma duniani. Pia ni tishio baya la dharura kwa afya ya wanyama na mimea, kwa utosheleshaji wa chakula na kwa maendeleo ya kiuchumi. 

Mambo mapya katika ripoti

Ripoti inalenga kufichua na kubainisha vipengele tofauti, vinavyoingiliana, vipengele vya mazingira vya AMR, kwa kutoa maelezo ya jumla kwa kina wa matokeo ya kisayansi kuhusiana na mada hii.  Inatoa ithibati ya mambo yanayoweza kutekelezeka kuhusu umuhimu wa mazingira kwa ukuzaji, uenezaji na usambasaji wa AMR, na  inaonyesha kuwa vipengele vya mazingira vya AMR vina pande nyingi na  kuvishughulikia kunategemea ushirikiano kati ya sekta mbalimbali.  Mbinu ya ushirikiano kama vile mkakati wa Afya Moja, ambao unatambua kuwa afya ya watu, wanyama, mimea na mazingira ina uhusiano wa karibu na hutegemeana, ndiyo mbinu inayohitajika kukabiliana na hali hii.

Ripoti hii inachanganua sekta tatu za kiuchumi na mifumo yake ya utendakazi ambayo ni vichochezi vikuu vya ukuzaji, na uenezaji wa AMR kwa mazingira: makampuni ya dawa na kemikali nyinginezo, kilimo na chakula, na huduma ya afya, pamoja na vichafuzi kutokana na kutozingatia usafi, maji taka na taka katika mifumo ya manispaa. Ripoti inaangazia mapungufu ya maarifa kwa sasa, na inaonyesha kuwa ingawa hatua kadhaa zinaendelea kuchukuliwa, hatua zaidi zinahitajika inatoa suluhisho la kushughulikia AMR.   

Suhuhisho la Afya Moja kwa AMR halitasaidia tu kupunguza hatari na mzigo wa AMR kwa jamii lakini pia litasaidia kushughulikia changamoto za aina tatu duniani.