Ripoti ya Ufuatiliaji wa Upunguzaji wa Joto Duniani, Kudumisha Ubaridi: Jinsi ya kukidhi mahitaji ya kupunguza joto huku tukipunguza uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa muungano wa Cool Coalition unaoongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa – inaainisha hatua endelevu katika maeneo matatu: mifumo ya kupunguza joto isiyohitaji ukarabati, viwango bora vya kutumia nishati vizuri na hatua za dharura za kuachana na friji zinazoongeza joto. Ripoti hii inayotolewa ili kuunga mkono Ahadi za Kupunguza Joto Duniani, mpango wa pamoja kati ya Muungano wa Cool Coalition na Umoja wa Falme za Kiarabu kama mwenyeji wa COP28.