Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ufadhili wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi unapaswa kuimarishwa kwa dharura. Makadirio ya gharama za kukabiliana na gesi chafu katika nchi zinazoendelea ni kubwa mara tano hadi kumi zaidi kuliko mtiririko wa sasa wa fedha za umma za kukabiliana na gesi chafu, na pengo la ufadhili wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi linaongezeka.
Fursa ya kutumia hela za kujiimarisha baada ya janga la COVID-19 kufadhili mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pia inapotea. Chini ya theluthi moja ya nchi 66 zilizofanyiwa utafiti zimefadhili wazi mikakati ya kukabiliana na COVID-19 ili kushughulikia madhara kwa mazingira kufikia Juni mwaka wa 2021. Hatimaye, kuongezeka kwa gharama ya kulipa madeni, pamoja na kupungua kwa mapato ya serikali, vinaweza kuathiri matumizi ya fedha za serikali ya kukabiliana na gesi chafu katika siku zijazo.
Uzuri ni kuwa, kukabiliana na na mabadiliko ya tabianchi kunazidi kujumuishwa kwenye sera na mikakati. Angalau asilimia 79 ya nchi zimepitisha angalau mkakati mmoja wa kitaifa wa kukabiliana na gesi chafu - ongezeko la asilimia 7 tangu mwaka wa 2020 Utekelezaji wa hatua za kukabiliana na gesi chafu unaendelea kuongezeka polepole, huku wafadhili kumi wakuu wakifadhili zaidi ya miradi 2,600 inayolenga kukabiliana na uzalishaji wa gesi chafu kati ya mwaka wa 2010 na mwaka wa 2019.
Kwa ujumla, ripoti hiyo inaonyesha kuwa juhudi zaidi zinahitajika ili kupiga hatua katika ngazi ya taifa kuweka mikakati, kuifadhili na kuitekeleza kote ulimwenguni.