Ni yepi mapya katika ripoti ya mwaka huu?
Ripoti hii – inayoangazia hatua zilizopigwa kutokanana juhudi za mikakati, ufadhili na utekelezaji wa kukabiliana na hali – inaonyesha kuwa mahitaji ya kifedha ya kukabiliana na hali katika nchi zinazoendelea sasa ni kati ya mara 10 na 18 zaidi kwa kuzingatia mtiririko wa kimataifa wa fedha za umma Hii ni zaidi ya asilimia 50 kuliko viwango vya makadiliro ya awali.
Gharama za miradi ya kukabiliana na hali hii katika nchi zinazoendelea zinakadiriwa kuwa dola za Marekani bilioni 215 kwa mwaka katika muongo huu. Fedha za kukabiliana na na mabadiliko ya tabianchi zinazohitajika ili kutekeleza vipaumbele vya kukabiliana na hali vya taifa zinakadiriwa kuwa dola za Marekani bilioni 387 kwa mwaka.
Licha ya mahitaji haya, mtiririko wa fedha za kukabiliana na hali za mashirika ya kimataifa na baina ya nchi mbili kwa nchi zinazoendelea ulipungua kwa asilimia 15 hadi dola bilioni 21 katika mwaka wa 2021. Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya kifedha ya kukabiliana na hali na kupungua kwa pesa zinazopokelewa, hali ya sasa ya pengo la ufadhili linakadiriwa kuwa dola za Marekani kati ya bilioni 194 na bilioni 366 kwa mwaka. Wakati uo huo, mikakati na utekelezaji wa juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inaonekana kuwa mibovu. Kushindwa huku kukabiliana na hali kuna athari kubwa kwa hasara na uharibifu, haswa kwa walio hatarini zaidi.
Ripoti hii inabainisha njia saba za kuimarisha ufadhili, ikiwemo kupitia matumizi ya ndani ya nchi na ufadhili wa kimataifa na wa sekta binafsi. Njia za ziada ni pamoja na fedha kutoka nje, kuongeza na kutoa ufadhili kwa Mashirika ya Biashara Madogo na ya Kati kutegemea hali na kufanyia mabadiliko mfumo wa ufadhili duniani. Mfuko mpya wa kugharamia hasara na uharibifu utahitaji kuzingatia mbinu bunifu zaidi za ufadhili ili kufikia kiwango kinachohitajika cha uwekezaji.