Msururu wa Ripoti ya UNEP ya Kukabiliana Na Pengo la Juhudi za Kukabiliana na Uzalishaji wa Gesi Chafu (AGR) inatoa kila mwaka tathmini ya kisayansi ya hatua zilizopigwa duniani za mikakati, ufadhili, utekelezaji wa juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia inaangazia jinsi ya kuimarisha na kuendeleza juhudi za kukabiliana na hali za kitaifa na kimataifa na kutoa uchanganuzi wa kina wa masuala muhimu mahususi. UNEP imekua ikitoa ripoti ya AGR tangu mwaka wa 2014, na lengo la kutoa taarifa kwa mazungumzo ya kushughulikia tabianchi katika Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa. Ingawa inasalia kuwa tathmini inayojitegemea, lengo la AGR linawiana kwa karibu na lile la Tathmini ya Kimataifa ya UNFCCC. AGR huandaliwa kwa ushirikiano na UNEP, Kituo cha Tabianchi cha Copenhagen cha UNEP (UNEP-CCC) na Mpango wa Kisayansi wa Kukabiliana na Tabianchi (WASP).