Ni yepi mapya katika ripoti ya mwaka huu?
Ripoti hii imegundua kuwa hatua za ufadhili wa kukabiliana na hali hazipigwi kwa kasi ya kutosha ili kuziba pengo kubwa kati ya mahitaji na mtiririko wa fedha, jambo ambalo linachangia kuendelea kuregarega kwa juhudi za upangaji na utekelezaji wa kukabiliana na hali.
Mitiririko ya fedha za kimataifa za umma za kukabiliana na hali kwa nchi zinazoendelea uliongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 22 katika mwaka 2021 hadi dola za Marekani bilioni 28 katika mwaka wa 2022: ongezeko kubwa kabisa la mwaka baada ya mwaka tangu wakati wa Mkataba wa Paris. Hali hii inaakisi maendeleo kuelekea Mkataba wa Tabianchi wa Glasgow, ambao ulihimiza mataifa yaliyoendelea angalau yaongeze maradufu fedha za kukabiliana na hali kwa nchi zinazoendelea kutoka takriban Dola za Marekani bilioni 19 (viwango vya mwaka wa 2019) kufikia mwaka wa 2025. Hata hivyo, hata kufikia lengo la Mkataba wa Tabianchi wa Glasgow kunaweza tu kupunguza pengo la kifedha la kukabiliana na hali, ambalo linakadiriwa kuwa dola za Marekani kati ya bilioni 187 na bilioni 359 kwa mwaka, kwa takribani asilimia 5.
Ripoti hii inatoa wito kwa mataifa kuimarisha ukabilianaji wa hali kwa kupitisha lengo jipya thabiti la takwimu za pamoja kuhusu ufadhili wa tabianchi na kujumuisha vipengele madhubuti vya kukabiliana na hali katika awamu inayofuata ya ahadi zao za kushughulikia tabianchi, au michango inayoamuliwa na taifa, inayotarajiwa mapema mwaka wa 2025.
Kwa kuzingatia ukubwa wa changamoto, kuziba pengo la fedha za kukabiliana na hali pia kutahitaji mbinu bunifu ili kukusanya rasilimali za ziada za kifedha. Kuimarisha vipengele wezeshi ni muhimu ili kuvutia ufadhili bunifu wa kukabiliana na hali. Uwekezaji katika katika ukabilianaji wa hali kimkakati na mabadiliko chanya ambavyo ni mgumu zaidi kufadhili pia utahitajika. Ufadhili wa ushugulikiaji wa hali unahitaji kuacha kukabiliana na matokeo, na kuwa unaongezeka, na unaozingatia tu mradi na kuanza kuwa unaokadiria zaidi, wa kimkakati na wa mabadiliko chanya.
Mbali na fedha, kuna umuhimu wa kuimarisha ujengeaji uwezo na uhamishaji wa teknolojia ili kuboresha ufanisi wa hatua za kukabiliana na hali. Ripoti hii inatoa mapendekezo ya kuboresha juhudi, ambazo mara nyingi haziratibiwi, ni ghali na za muda mfupi.
Kwa ujumla, juhudi zaidi zitahitajika ili kufikia lengo la kimataifa la kukabiliana na hali kupitia shabaha kumi na moja za Mfumo wa Kustahimili Tabianchi Duniani wa UAE.