01 Oct 2020 Tukio Kutumia mazingira kushughulikia tabianchi

Safari mpya inayoendeshwa mtandaoni inaonyesha umuhimu wa mboji

Kwa mjibu wa tathmini ya hivi karibuni kutoka kwa Jukwa la Kimataifa la Sera ya Sayansi kuhusu Huduma za Mifumo ya Ekolojia, asilimia 75 ya ardhi, asilimia 66 ya bahari na asilimia 85 ya maeneo oevu yameaithiriwa vibaya mno kutokana na shughuli za binadamu. Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha athari ya changamoto za mazingira na kuonyenya kuwa tunaweza kufeli kubimarisha uwezo wa sayari yetu kutuhudumia ipasavyo.

Kupata maarifa kuhusu jinsi mazingira yanavyofanya kazi kutuhudumia, kampeni ya Wild for Life 2.0 ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) itaelimisha watumiaji wake kupitia safari yake kuhusu mifumo minne ya kipekee- baharimbojisavana na misitu-umuhimu wake kwa maisha ya binadamu, na kwa nini i hatarini na wanachoweza kufanya ili kusaidia.

https://youtu.be/tHn6QOVEZQU

 

Safari hii inajumuisha mifumo ya kipekee: Mboji, inayochuja maji safi, kukuza mimea inayotumiwa kama dawa, kulinda ardhi dhidi ya mafuriko na kuteka na kuhufadhi kiwango kikubwa cha kaboni. Ijapokuwa mboji hukalia tu asilimia 3 ya ardhi, huhufadhi kiwango cha kaboni maradufu ikilinganishwa na misitu yote duniani ikijumuishwa!

Kuweko kwa safari ya Wild for Life 2.0 ya Mboji  ni muhimu kote duniani kwa maeneo ya mboji kama vile Mboji za Peninsula Mitre inayopatikana katika Ncha ya Kusini mwa Amerika Kusini. Tierra del Fuego archipelago eneo la kusini mno mwa mboji ya Magellanic (moorland). Kisiwa kikuu, Isla Grande de Tierra del Fuego, kiko kati ya magharibi mwa Chile na mashariki mwa Argentina. Hali ya bahari na upepo wa Kusini Magharibi hutokea kusini mwa Tierra del Fuego, eneo la mashariki ya magharibi lililo na mandhari yaliyo na milima mingi.

UNEP inazungumza na msimamizi wake wa Maeneo Yaliyohifadhiwa, Kristine Tompkins, na msimamizi wa Bahari, Lewis Pugh kuhusu umuhimu wa mboji. Wote wamewahi kutembea eneo hili la dunia na wako katika mstari wa mbele kuhamasisha kuhusu maeneo yaliyohifadhiwa, kupitia wakfu za Tompkins na Lewis Pugh.

UNEP: Kristine, umehifadhi na kukuza wanyamapori katika mamilioni ya hekari nchini Chile na nchini Argentina. Ni nini kilichokuchochea kufanya hivyo?  

Kwa kweli, mnamo mwaka wa 1992, mme wangu Douglas Tompkins ndiye aliyetambua kuwa tunaweza kushiriki katika vuguvugu la kimataifa la hifadhi kwa kubuni miradi ya hifadhi kwa ushirikiano na watu binafsi na na umma kwa lengo la kuanzisha mbuga mpya za wanyawa nchini Chile na nchini Argentina.  Kwa hivyo, tunaweza kusema kuwa nilishawishiwa na uwezo wa mme wangu wa kufikiria kuhusu kuanzisha maeneo makubwa yaliyohifadhiwa daima. Tangu tulipoanza, Hifadhi yaTompkins haijachelea kubuni maeneo mapya ya kuhifadhia wanyamapori na kuyajaza na wanyamapori katika nchi husika.

UNEP:  Lewis umehamasisha kuhusu kutunza bahari katika Maeneo ya Polar. Mbona huwa unahatarisha maisha yako kufanya hivyo.

Kwa zaidi ya miaka 30 nimekuwa nikiogelea baharini, na nimeona mabadiko makubwa katika bahari hizo. Mabadiliko makuu yameshuhudiwa katika Maeneo ya Polar ambapo nimeshuhudia ongezeko la joto baharini, kupungua kwa barafu, kuyeyuka kwa theluji na kutokomea kwa barafu ya baharini. Mabadiliko haya yataathiri kila mtu na wanyama wote. Mabadiliko ya tabianchi yataongezeka kwa kasi iwapo hatutatunza mifumo muhimu ya ekolojia kama vile mboji, ambayo huwa inateka kiwango kikubwa cha kaboni. Siwezi nikatulia hali inapoendelea ilivyo.

UNEP: Ulijuaje kuhusu eneo hili lilioko vijijini na hata kulipenda?

Kristine:  Douglas alipokuwa anafanya mazoezi ya skii mwanzoni mwa miaka ya 1960 katika nchi za Argentina na Chile aliweza kuelewa eneo  la Ncha ya Kusini vyema. Nilimfuata miaka ya 1960, na sote tulipenda eneo hili, ila cha muhimu mno, tuliona kuwa lilikuwa na mandhari mbalimbali, kuanzia kwa misitu ya mvua inayojulikana kwa sasa kama Mbuga ya Kitaifa ya Wanyama ya Pumalin Douglas Tompkins hadi kwa maeneo mapana yaliyo na nyasi ya Patagonia. Hivi majuzi, wakati tunaposhuhudia mabadiliko mabaya ya tabianchi, tunaangazia umuhimu wa mboji, hasa katika maeneo ya Tierra del Fuego nchini Chile na Argentina. Kwa mfano, Peninsula Mitre, eneo lililo na takribani asilimia 84 ua mboji inayopatikana nchini Argentina, ni muhimu mno kwa kuteka kaboni nyingi nchini.  

Lewis: Safari zangu nyingi katika eneo la Antaktiki huwa Patagonia. Huko ndiko huwa nafanyia mazoezi ya mwisho majini. Beagle Channel ni eneo mwafaka la kufanyia mazoezi ya kuogelea kwenye Antaktiki. Maji yake ni baridi kama barafu, ila siyo baridi mno kiwango cha kushindwa kufanya mazoezi. Barafu ya Darwin, eneo ambalo theluji yake huonekana baharini katika maeneo ya Beagle Channel na Straits za Magellan, hupatikana hapa.

Kila wakati ninaposafiri kupitia Patagonia, huwa ninajiambia kuwa ninahitaji kukaa hapa zaidi, kutokana na umaridadi wake. Ninaunga mkono kuunganishwa kwa maeneo yaliyohifadhiwa ardhini na baharini kama vile mapendekezo yanayotolewa kuhusu maeneo ya mboji ya Peninsula Mitre.

UNEP:  Ni kipi cha kupigiwa upato kwa yale yote uliyotenda?

Kristine: Aaah, ni vigumu kutaja!  Kwa hakika, mchango wa mwisho uliotolewa kwa mbuga ya kitaifa miezi kumi na nane iliyopita nchini Chile, mchango mkubwa mno kuwahi kutolewa kwa shughuli za hifadhi, ni moja wapo. Ila, tuna furaha kwa kufikia mengi ya malengo yetu makuu ya shughuli za hifadhi kwa kipindi cha miaka 28. Najivunia vikosi vyetu na uhusiano ambao tumejenga na serikali kupitia kila shughuli!

Lewis: Ni muhimu kuanzisha Eneo la Bahari Lililohifadhiwa kwenye Antaktiki. Nilipoogelea hapa katika mwaka wa 2015, kuonyesha umuhimu wa kutunza bahari hii, ilikuwa vigumu mno - bila kusahau kuwa ni baridi mno! Baadaye, nilisafiri kati ya miji mikuu mbalimbali kwa kipindi cha miaka miwili ili kuhakikisha makubaliano yanaidhinishwa. Ilikuwa safari ya kuchosha. Lakini Bahari ya Ross ni mojawapo ya mifumo muhimu ya ekolojia duniani. Na kilomita milioni 1.5 mraba, MPA ya Bahari ya Ross ndilo eneo kubwa mno kuhufadhiwa duniani. Kufafanua zaidi, linatoshana na Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Italia zikiunganishwa.

UNEP:  Watu wa kawaida wanaweza kufanyaje ili mashirika yao yalete mabadiliko ya kudumu?

Kristine: Mwanzo, na hatua iliyo ngumu mno, ni kuamua kujiunga na vuguvugu la kuleta mabadiliko kuhusiana jinsi tunavyoishi kwa mazingira, ili kuwa na jamii dhabiti iliyo na afya njema. Bila kujitolea kwa namna hii, tutarudia hali ya kutofanya chochote haraka mno.

Kama mambo mengine yote duniani, ni sharti mtu ajitolee pasi kuchoka - kwa mfano, kuamka kila siku na kufanya mambo unayoyapenda, mambo unayoyaamini. Kuna mamilioni a watu wanaofanya shuguli za uhifadhi na kila mmoja wetu ni mtu wa kipekee, ila tunajitolea kufanya tuwezayo. Hatuwezi kutulia tu!

Lewis: Uanze kwa kujielimisha kuhusu masuala ya mazingira ili kuweza kuelewa athari ya matendo yetu kwa sayari yetu. Kwa mfano, chochote unachonunua ni uamuzi kuhusu mustabali unaotaka kwa wanao. Chakula tunachokula, nguo tunazovaa, jinsi tunavyosafiri, jinsi tunavyojenga na kupika majumbani- vyote vina athari zake.

Pia, ninamini kuwa ni muhimu kutumia mda wako katika mazingira. Sisi hutunza tu vitu tunavyovipenda, na ni sharti upenda mazingira asilia unapochukua mda wako kuelewa kuwa hutokea kumuujiza.

UNEP:  Kwa sasa mnafanya nini kikuu?

Kristine: Tuna miradi mingi mipya ya kutunza ardhi na bahari inayoendelea nchini Chile na Argentina. Isitoshe, bado tunajitolea kuhakikisha baadhi ya miradi iliyoanzishwa hapo awali inafaulu.  Mara nyingi, sisi huulizwa, "Ni kipi kitakachofuata?", na ningependa kukuambia kuwa changamoto za mazingira na uwezekano wa viumbe kuangamia ni mambo yanayopaswa kushughulikiwa kwa dharura kwa sababu huongezeka kila uchao. Ni sharti tuchukue hatua haraka, kwa kiwango kikubwa na kwa kujitolea zaidi.

Lewis: Kwa sasa, kikosi changu nikiwemo tunajitolea kuunda mtandao wa maeneo ya bahari yaliyohifadhiwa kwenye Antakitiki ili kulinda eneo hilo dhidi ya uvuvi wa samaki wa biashara kupindukia, hali inayoshudiwa kwenye bahari zinginezo, na kusaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Maeneo haya yaliyohifadhiwa yatapatikana Mashariki mwa Antiktiki, Bahari ya Weddell na Antaktiki ya Peninsula. Pamoja na MPA ya Bahari ya Ross, yatahifadhi eneo la zaidi ya kilomita 4 mraba la bahari lililo hatarini. Itahitaji kazi nyingi na ushawishi mwingi kwa sababu sababu mataifa 25 yanayosimia Antaktikai, ni sharti yote yakubali kushiriki. Ila nimejitolea kwa dhati kuhakisha maeneo mengi duniani yanahifadhiwa ipasavyo.