08 December 2023 Ripoti

Ni kipi kinachoendelea? Tathmini ya athari zinazoweza kutokea kutokana na masuluhisho mapya yaliyochaguliwa badala ya bidhaa za kawaida kuto...

Waandishi: UNEP
Jalada

Mifumo ya chakula huchangia takriban asilimia 30 ya uzalishaji wa sasa wa GHG za nthropojeniki, na bidhaa kutoka kwa wanyama huchangia angalau asilimia 60 ya uzalishaji huo. Kuna umuhimu wa kubadili jinsi tunavyozalisha na kutumia chakula tunachokula, kutokana na kuongezeka kwa athari zake kwa changamoto za aina tatu duniani. Ingawa mbinu nyingi zipo za kushughulikia athari mbaya za kilimo cha ufugaji wa wanyama, ripoti hii inaangazia hasa bidhaa mbadala badala ya chakula cha kawaida kutoka kwa wanyama.

Toleo hili maalum la Ripoti ya Mipaka linaangazia athari zinazoweza kutokea kwa mazingira, afya, jamii na maslahi ya wanyama kutokana na utumiaji wa nyama na maziwa mbadala, haswa bidhaa mpya kutoka kwa mimea, kutokana na uchachushaji mimea inayokuzwa. Kikosi cha wataalam wa nyanja mbalimbali kimetathmini ushahidi unaopatikana kuhusu athari za bidhaa hizi mbadala kwa kulinganisha na bidhaa za kawaida, na kubainisha masuala muhimu ya kuzingatiwa na watungasera wanaohusika na kudhibiti, kuwekeza au kutoa usaidizi mwingine kwa bidhaa zmpya za nyama na maziwa na kuangazia maeneo zaidi yanayohitaji utafiti.

Ni kipi kinachoendelea: Toleo maalum la UNEP la Ripoti ya Mipaka ya Mwaka wa 2023

Toleo hili maalum la UNEP la Ripoti ya Mipaka linaangazia ushahidi uliopo kwa bidhaa vipya vinavyotokana na mimea, nyama inayotengenezwa na uchachushaji wa mimea inayokuzwa kama bidhaa mbadala au vya kukamilishana na nyama na maziwa ya kawaida na kuwa na uwezekano mdogo wa kuchafua mazingira. Ripoti hii inatoa maarifa ya kisayansi ya bidhaa hizi mpya mbadala kama mbinu ya kuleta…

Kutumia bidhaa mpya mbadala badala ya nyama na maziwa kunaweza kusaidia kupunguza uzalishaji wa hewa chafu inayodhuru - Umoja wa Mataifa

Bidhaa mpya mbadala zinazoibuka badala ya bidhaa kutoka kwa wanyama kama vile nyama na maziwa zinaweza kuchangia pakubwa kupunguza athari kwa mazingira za mfumo uliopo kwa sasa wa chakula duniani, hasa katika nchi za kipato cha juu na cha kati, mradi zikitumia nishati ya kiwango kidogo cha hewa ya ukaa.

Unachohitaji kujua kuhusu vyakula mbadala vya asili ya wanyama

Kadiri idadi ya watu duniani inavyoongezeka, ndivyo mahitaji ya vyakula vinavyotokana na wanyama kama vile nyama na maziwa yanaongezeka. Changamoto: kilimo cha ufugaji wa wanyama kinaweza kuharibu mazingira, na kuzidisha changamoto za aina tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na mazingira, na uchafuzi na taka